Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
Naibu
Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na utawala bora
Dkt. Mary Mwanjelwa ametembelea ofisi za wakala wa mafunzo kwa njia ya
mtandao nchini (TaGLA) huku akitoa pongezi kwa wafanyakazi kwa kazi hiyo
wanayoifanya ambayo ni tofauti na yenye tija kwa jamii.
Akizungumza
mara baada ya kutembelea vitengo vya wakala hiyo Dkt. Mwanjelwa amesema
kuwa kazi zinazofanywa na wakala hiyo zina tija kwa wananchi na
Serikali na kuwataka kujitangaza zaidi ili wananchi waelewe majukumu
yanayofanywa na wakala hiyo.
Aidha
amewataka wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuzidi
kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais
Dkt.John Joseph Magufuli.
Amesema
kuwa wizara anayoisamia ipo tayari kushirikiana nao katika shughuli
zao ambazo nyingi zimelenga kuokoa gharama za Serikali.
Kwa
upande wake Mkurugenzi mkuu wa wakala hiyo Charles Senkondo amesema
kuwa tangu kuanzishwa kwa wakala hiyo miaka 18 iliyopita wamekuwa na
jukwaa la TEHAMA linalohusisha wanajamii mbalimbali.
Senkondo
amesema kuwa majukumu ya wakala hiyo ni pamoja na kutoa mafunzo kwa
watumishi wa umma na sekta binafsi kwa kutumia mifumo ya kiteknolojia
ikiwemo video Conference ambayo huwakutanisha watu tofauti kwa wakati
mmoja hali inayopelekea kupunguza gharama.
Senkondo
amesema kuwa wakala hiyo pia inatoa huduma za mikutano ya kazi na zile
za daraja video, midahalo huduma za maabara ya kompyuta.
Amesema
kuwa wamejipanga katika kuhakikisha huduma hiyo inafika katika Mikoa
yote nchini na tayari wamewasiliana na wizara ya mambo ya nje na
uhusiano wa kimataifa katika kushirikiana na sekta mbalimbali zikiwemo
TANTRADE, TIC na madaktari bingwa katika kuwajengea uwezo.
Aidha
amesema kuwa wana malengo ya kutoa mafunzo ya matumizi ya TEHAMA na
kuendesha vikao vya kazi kwa watumishi wa umma na taasisi binafsi ili
kuwajengea uwezo na kuwafikia wafanyakazi hao kwa muda mfupi na kuokoa
gharama.
Vilevile
Senkondo amesema kuwa wamefanya midahalo mingi na nchi nyingine
zikiwemo Korea kusini na kenya na kujadili masuala mbalimbali ya kijamii
kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na ukuaji wa miji kupitia mfumo wa
daraja video huku akimpongeza Naibu waziri wa Viwanda na biashara
Mhandisi Stella Manyanya kuwa balozi bora wa wakala hiyo.
Mkurugenzi
mkuu wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini Charles Senkondo
akieleza majukumu ya wakala hiyo mbele wa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa
mara baada ya kukagua utendaji kazi unaofanywa na wakala hiyo jijini
Dar es Salaam.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na watumishi mara baada ya Mkurugenzi
mkuu wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini Charles Senkondo
kuwasilisha majukumu ya wakala hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Meneja
mafunzo na habari kutoka wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao TaGLA
Dickson Mwanyika akitoa mwongozo katika warsha hiyo iliyofanyika katika
ofisi za wakala hiyo, jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na watumishi wa ofisi yake jijini
Dodoma alipotembelea ofisi za TaGla leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao TaGLA wakiwa
kwenye mkutano na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa alipotembelea ofisihizo jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na wafanyakazi wa wakala wa mafunzo kwa
njia ya mtandao TaGLA mara baada ya kukagua utendaji kazi unaofanywa na
wakala hiyo huku akieleza kufurahishwa na utendaji kazi wao, jijini
Dar es Salaam.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Dkt. Mary Mwanjelwa akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Mkurugenzi
mkuu wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini Charles
Senkondo jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Dkt. Mary Mwanjelwa akionesha zawadi aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa
wakala hiyo Charles Senkondo, jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
TaGLAjijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment