Somo la jaji Sammata kwa wanasheria kukomesha kabisa kansa ya rushwa
Taasisi
ya Wajibu nchini inayoshughulika na fikra ya uwajibikaji kwa umma
imeendelea kutoa mafunzo kwa watu wa kada mbalimbali kuhusiana na
masuala ya uwajibikaji na uadilifu.
Moja
ya midahalo mikubwa ni ile iliyotolewa na jaji mkuu mstaafu na mkuu wa
chuo cha Mzumbe Barnabas Sammata katika Chuo kikuu cha Dodoma na Chuo
cha sheria nchini kilichopo jijini Dar es salaam na katika midahalo hiyo
jaji Sammata alitoa mada kuhusiana na mapambano dhidi ya rushwa kwa
kueleza kuwa rushwa ni kansa inayosababisha kutoweka kwa imani ya raia
juu ya demokrasia .
Akiwa
katika chuo cha sheria jaji Sammata aliaishukuru taasisi ya wajibu na
uongozi wa chuo cha sheria kwa heshima waliyompa hasa kwa kutoa mada na
kuwanoa wanasheria hao kuhusiana na mapambano dhidi ya rushwa ambayo
imekuwa adui zaidi kwa ustawi wa wananchi wakati wa amani kuliko wakati
wa vita.
Jaji
Sammata alieleza kuwa rushwa katika nchi inatakiwa ishughulikiwe kwa
karibu sawasawa na inavyoshughulikiwa suala la uhaini na vijana lazima
wawe mstari wa mbele katika kupinga rushwa.
Sammata
alieleza kuwa ili kukabiliana na kansa ya rushwa lazima ofisi ya
Mkurugenzi wa mashtaka na TAKUKURU kuhakikisha nini kifanyike ili
kumwokoa mnyonge kutoka kwenyejanga hilo.
"Rushwa
si kansa iliyoanza jana au juzi,kwa mujibu wa biblia ilikuwepo tangu
wakati wa yesu miaka ipatayo zaidi ya elfu mbili iliyopita, Korani
inakemea sana uovu huo" alieleza Sammata huku akisema kuwa sababu za
kupokea rushwa ni nyingi ikiwemo kuharakisha kupata huduma, kupata zaidi
ya unachostahili pamoja na kupata kile ambacho mtu ana haki nacho.
Vilevile
alieleza madhara ya rushwa ambapo Jaji Sammata alisema kuwa kansa hiyo
ni kuwanyang'ganya wananchi haki yao hasa matarajio yao ya baadaye
ikiwemo maisha bora na maendeleo waliojiwekea, alisema kuwa rushwa
hujenga chuki kwa kuwa huvunja haki na waathirika huchukua sheria
mkononi wakiona vyombo husika havijatenda haki.
Jaji
Sammata alitoa maoni yake na kusema kuwa ili kuepuka hayo yote lazima
elimu zaidi kwa umma itolewe na kushauri vyama vya siasa hasa chama
tawala na vyombo vya dola kukemea vitendo hivyo huku akihimiza taasisi
za dini zishiriki katika kupinga kampeni hiyo kwa kutoruhusu mapato ya
rushwa kutunisha kampeni hizo.
Aidha
katika mdahalo huo aliwataka wanasheria nchini kote kuwa mstari wa
mbele katika kupinga vitendo hivyo na kuwa waaminifu bila kujali
ukubwa au udogo wa rushwa ambayo zinaathiri maendeleo ya jamii huku
akisisitiza watakaokiuka taratibu za kisheria hata wakiwa waandishi wa
habari ambao watakutwa na vitendo hivyo katika kazi zao wachukuliwe
hatua kali kwa kuwa wao ndio ngao muhimu katika kumulika vitendo hivyo.
Katika
mdahalo huo mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya WAJIBU ambaye pia
ni mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)Ludovick Utouh
alisema kiwa taasisi hiyo ni changa na kuanzishwa kwake kulisababishwa
na kulegalega kwa uwajibikaji na uadilifu na alihaidi kuendelea
kuwafikia walengwa kadri watakavyoweza huku wakiwalenga wanafunzi wa
vyuo ambao ndio viongozi watarajiwa.
No comments:
Post a Comment