Afisa
Mradi wa kupinga ukatili wa Kijinsia katika masoko ya Mbagala Rangitatu
na Kampochea ujulikanao kama Mpe Riziki si Matusi, Shabani Rulimbiye
(kushoto), akitoa mada wakati akitoa mafunzo ya namna ya kujikinga na
ukatili wa kijinsia kwa maofisa wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.Mafunzo hayo ya siku moja yaliandaliwa na
Shirika la Equality for Growth (EfG).
Afisa
Ustawi wa Jamii, Getruda Nyagabona (kushoto) kutoka Manispaa ya Temeke
akizungumza katika semina ya siku moja ya namna ya kupinga ukatili wa
kijinsia masokoni iliyoandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa
Ustawi wa Jamii, Magrida Mumba.
Washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada kwa makini.
Mwenyekiti wa Soko la Kampochea, Hemed Said Njiwa akichangia jambo.
Majadiliano katika makundi.
Majadiliano wa kazi za makundi.
Ofisa Mtendaji wa Mbagala Rangitatu, Morris Ssendi (kushoto), akichangia jambo wakati wa kazi za makundi.
Afisa Ustawi wa Jamii, Magrida Mumba, akichangia jambo.
Katibu wa Soko la Mbagala Rangitatu, Frank Mapolu akichangia jambo kwenye semina hiyo.
Na Dotto Mwaibale
Halmashauri za miji zimetakiwa kuboresha miundombinu ya masoko kwa kuwa yanachangia
asilimia kubwa ya pato la Serikali za mitaa nchini.
Ombi
hilo limetolewa na Afisa Mradi wa kupinga ukatili wa Kijinsia katika
masoko ya Mbagala Rangitatu na Kampochea ujulikanao kama Mpe Riziki si
Matusi, Shabani Rulimbiye unaoendeshwa na Shirika la Equality for Growth
(EfG) wakati akitoa mafunzo ya namna ya kujikinga na ukatili wa
kijinsia kwa maofisa wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki.
Maofisa
walionufaika na mafunzo hayo ni maofisa ustawi wa jamii,maendeleo ya
jamii, watendaji wa kata, askari polisi kutoka dawati la jinsia na
viongozi `wa masoko.
Alisema
masoko mengi ambayo yanaendeshwa na sekta binafsi ambayo imetoa ajira
mara tano ya ajira zilizo sekta rasmi na kuokoa wanawake wengi na watoto
wao miundombinu yake ni mibovu na hayajawekewa sera na usimamizi wa
kisheria kuanzia mazingira ya kazi, kipaumbele kwa makundi maalumu na
zaidi ukatili wa `kijinsia `uliokithiri.
"Pamoja
na kua ni kimbilio la wahanaga wa mfumo dume, sekta hii pia ni chachu
kubwa sana ya maendeleo ya mwanannchi binafsi, serikali za mitaa na
Taifa kwa ujumla ambapo takwimu zinaonesha kuwa Halmashauri zinategemea
zaidi masoko kwa kuchangia kipato" alisema Rulimbiye.
Aliongeza
kuwa pamoja na sekta hii isiyo rasmi kuwa ni chanzo kikubwa cha ajira
na kuchangia asilimia kubwa ya pato la Taifa, mazingira yake yanafanywa
kama chaka la utovu wa nidhamu na wahanga wakubwa ni wanawake, ambao ni
wengi ambao pia wakati mwingine hujumuika na watoto wao.
Afisa
Ustawi wa Jamii, Getruda Nyagabona alisema kesi nyingi za ukatili wa
kijinsia zimekuwa zikitatuliwa kwa ushiriano baina yao na viongozi
mbalimbali kuanzia ngazi ya chini jambo ambalo limesaidia kupunguza
vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment