Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema
kuwa bunge limejipanga kuishauri serikali kutekeleza azimio la Malabo
la kutenga Asilimia 10 ya bajeti kwa ajili ya usalama wa chakula na
suala la lishe bora kwa jamii.
Akizindua jukwaa la majadiliano ya Usalama wa chakula ya mabunge ya
Afika mashariki na kusini iliyoandaliwa na Bunge la Afrika mashariki
Ndugai alisema kuwa changamoto kubwa kwenye sekta ya kilimo bado
bajeti yake haijatekelezwa kwa asilimia japo 30 hivyo kwa kuanzia
angalau kwenye bajeti za maendeleo za nchi zetu tukaanzia na asilimia
10
Amesema kuwa pamoja na serikali kujitahidi bado kunachangamoto kubwa
ya lishe duni na udumavu katika jamii hivyo kama tunataka kufikia
kwenye maendeleo ya kiuchumi tunahitajika kujenga miundombinu ya
kufikika kwa wakulima wetu sanjari na kuhimiza kilimo na ufugaji kwa
kutenga bajeti inayoakisi kufikia huko.
“Changamoto ninaoyoiona leo kwetu kama nchi za bara la afrika ni
kutoona umuhimu wa kujipanga kutekeleza azimio la Malabo baada ya
viongozi wetu wa mataifa ya bara hili kuipitisha mwaka 2014 kuhusu
usalama wa chakula hivyo muhimu kama nchi zetu kuweka maazimio kama
mabunge linalotaka kila nchi kwenye bajeti yake ikaweka asilimia 10
kwa ajili ya sekta ya kilimo mifugo na uvuvi”alisisitiza Ndugai.
Kwa Upande wake Mbunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Asha Abdallah Juma(Mshuwa)ameipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa
kuwa na usalama wa chakula ili kuondoa tatizo la udumavu kwa watoto
kwa kukosa lishe bora kwenye miaka mitatu ya mwanzo.
Amewataka wa Bunge kutotunga Sheria pekee na wajikite kuwa na mashamba
ya mfano Kwa wananchi wanaowaongoza kuibua uzalishaji na kilimo kikue
hapo tutapata maendeleo ya kiuchumi.
"Sisi Kwa mfano tulianzisha chuo maeneo ya chukwani Kwa lengo la
kuwezesha jamii kutumia eneo dogo kuzalisha Kwa tija ili tunapopata
nafasi tuitumie vizuri kuzalisha chakula Kwa wingi"
Mshuwa alieleza kuwa warsha hizo ni nzuri Sana kwani zinasaidia nchi
zetu kuondoa changamoto zinazotukabili ikiwemo ukosefu wa Ardhi Kwa
ajili ya uzalishaji inayotufanya kutokuwa na usalama wa chakuli na
lishe duni.
Nae mbunge wa Babati vijijini Jituson alisema kuwa mkoa wa Manyara ni
wazalishaji wakubwa lakini udumavu bado ni changamoto kubwa kutokana
na ukosefu wa lishe Bora Kwa watoto wanaozaliwa hivyo kuiomba serikali
kuona umuhimu wa kuongeza bajeti yetu kwenye kilimo mifugo na uvuvi.
Ameitaka jamii kurudi Kula vyakula vya asili ambavyo havina wanga
mwingi na kuacha Kula vyakula ambavyo vitasababisha miili kukosa afya
Bora.
No comments:
Post a Comment