Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, (CGF) Thobias
Andengenye, amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa hapa
nchini.
Makamanda
walioguswa na mabadiliko hayo ni Kamishna Msaidizi wa Zimamoto (ACF)
Mohamed Kondo, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa
Kinondoni, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya.
Kamishna
Msaidizi (ACF) Juma Yange, aliyekuwa Kitengo cha Utawala Mkoa wa
Kinondoni, anakuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kizimamoto
Kinondoni.
Mrakibu
Msaidizi wa Zimamoto (ASF) John Francis, aliyekuwa Chuo cha Zimamoto na
Uokoaji Handeni Mkoani Tanga, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na
Uokoaji Mkoa wa Rukwa.
Vilevile,
aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma, Mrakibu
Msaidizi wa Zimamoto (ASF) Athumani Basuka, anaenda kuwa Kamanda wa
Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Hai – Siha, nafasi yake inachukuliwa na
Mrakibu Msaidizi (ASF) Jumbe Juma.
Pia
aliyekuwa Kamanda wa Kiwanja cha Ndege Mkoa wa Iringa, Mkaguzi wa
Zimamoto (INSP) Hamisi Dawa, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji
Mkoa wa Kagera.
Mabadiliko haya ni ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji linaendelea kutoa wito kwa Wananchi kuendelea
kutoa ushirikiano kwa Makamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mikoa na Wilaya
katika suala la Kinga na Tahadhari Dhidi ya majanga.
Imetolewa na;
Joseph Mwasabeja – (INSP)
Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Makao Makuu.
No comments:
Post a Comment