Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhe. Prof. Joyce Ndalichako leo
ametembelea na kukagua hatua za maandalizi ya ujenzi wa Jengo la
Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya, ambapo
amepongeza Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa hatua za ujenzi ulipofikia.
Akiwa
ameambatana na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Pro. Lughano Kusiluka, Prof
Ndalichako amemwelekeza Mkandarasi wa Ujenzi kuhakikisha kufikia Juni
2019 ujenzi wa Jengo hilo kuwa umekamilika kama ilivyopangwa.
Kukamilika
kwa ujenzi kutawezesha jumla ya wanafunzi 900 kupata vyumba vya
madarasa mbali na kumbi za mikutano na ofisi za uendeshaji. Jengo hilo
linatarajiwa kuwekwa jiwe la Msingi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt John Joseph Magufuli Mei 1, 2019.
Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako
akiongozwa na Mkandarasi wa mradi akikagua vyuma vya madarasa mara
alipowasili kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa tano la Taaluma na
Utawala linalotazamiwa kumalizika mwezi Juni,2019. Pamoja naye ni Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka, Naibu Mawakamu Mkuu
wa Chuo Utawala na fedha Prof. Ernest Kihanga na wasimamizi wa ujenziWaziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako
akiweka saini kwenye kitabu cha wageni kwenye eneo la ujenzi wa Jengo la
Taaluma na Utawala la chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya mbeya mara tu baada
ya kuwasili. Aliyeshika kitabu ni Injiani Thadeus Koyanga na kushoto
anayeshuhudia tukio hilo ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa
Lughano Kusiluka ( Mwenye Kaunda suti kushoto) Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako
(kushoto) akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano
Kusiluka ( Mwenye Kaunda suti kushoto) pamoja na Mkandararasi na
wajenzi; wakikagua ramani ya jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu
Mzumbe Kampasi ya Mbeya. Profesa
Ndalichako (katIkati) akikagua mahali litakapojengwa jiwe la msingi
ambalo litawekwa rasmi na Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muuungano wa Tanzania
Dr.John Pombe Joseph Magufuli Mei 1, 2019. Kushoto ni Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka na kulia ni Mkadarasi wa
Ujenzi Injinia Thedeus Koyanga (mwenye shati la mikono mirefu)
akifuatiwa na Profesa Ernest Kihanga Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala
na Fedha.Mhe.
Profesa Joyce Ndalichako alikagua muonekano wa nje wa jengo la Taaluma
na Utawala la chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya pamoja na kukagua usafi
wa mazingira, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi kabla
Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli hajafika kuweka jiwe la msingi.
No comments:
Post a Comment