Waziri
wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama amekagua maandalizi ya
Sherehe za Mei Mosi na kusema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa.
Ametoa
kauli hiyo Aprili 29, 2019 baada ya kupokea taarifa ya mbalimbali za
Kamati ya Maandalizi walipokutana kujadili na kupanga mipango katika
kuelekea kilele cha sherehe hizo zinazotarajiwa kuadhimishwa katika
Viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya.
Waziri
amesema Kamati ya Mkoa kwa kushirikiana na Ofizi yake imeendelea na
maandalizi hayo na kuendelea kutoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kufika
kwa wingi katika viwanja hivyo siku ya tarehe 1 Mei, 2019.
“Hadi
sasa maandalzi yamefikia hatua nzuri na watu wanafanya kazi kwa umoja
ili kuhakikisha shughuli hii inafana, wito wangu wananchi wajitokeze kwa
wingi kuja kuunga mkono wafanyakazi wa Tanzania katika siku yao hii
muhimu.”Alisema waziri Mhagama.
Waziri
aliwataka wanakamati hao wahakikishe wanasimamia vizuri wageni, pamoja
na shughuli zote zitakazofanyika uwanjani hapo ili kuhakikisha
wanaifikia siku hiyo kwa ushindi mkubwa.
Aidha
Waziri aliongezea kuwa, uwepo wa maadhimisho hayo Jijini Mbeya wanachi
wayatumie kama fursa ya kimaendeleo kwa kuwa mkoa utapokea wageni wengi
hivyo waendelee kuwahudumia vyema.
Aidha
kwa Upande wake rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.
Tumaini Nyamhokya aliendelea kuhamasisha wananchi hususan wafanyakazi
wote kujitokeza kwa wingi kuja kuiadhimisha siku hiyo.
“Ni
wakati sahihi kwa wafanyakazi wote nchini kuitumia siku hii maalum
katika kuiadhimisha na kuienzi ikiwa ni sherehe ya upekee sana hivyo
mjitokeze kwa wingi pamoja na wananchi wote kwa ujumla.”Alisisitiza
Nyamhokya.
Maadhimisho
ya Sherehe za Mei Mosi yatahadhimishwa Kitaifa katika Mkoa wa Mbeya
ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, aidha maonesho hayo yatapambwa na
shughuli mbalimbali ikiwemo; Maandamano ya wafanyakazi na magari, Kwaya
maalum, Nyimbo maalum kutoka kwa Vyama vya Wafanyakazi, wimbo maalum
kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya, vikundi vya ngoma kutoka mikoa
mbalimbali, Nyimbo maalum kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Kauli
mbiu ya maonesha ya mwaka huu inasema; “Tanzania ya Uchumi wa Kati
Inawezekana, Wakati wa Mishahara na Masilahi Bora kwa Wafanyakazi ni
SASA”
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akizungumza jambo kwa kamati ya
maaandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe ya Wafanyakazi za Mei Mosi
walipokutana nao kukagua maandalizi hayo katika Viwanja vya Sokoine
Jijini Mbeya Aprili 29, 2019.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akichangiua jambo wakati wa kikao hicho.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw.
Andrew Massawe akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
Mjumbe
Kamati ya Utendaji CWT Mwalimu Joyce Julius akichangia jambo katika
kikao cha maandalizi ya sherehe za Mei Mosi kilichofanyika katika
Viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya aprili 29, 2019.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akiangalia mazingira ya uwanja
wa Sokoine utakaotumika kwa ajili ya Maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi
kitaifa Jijini Mbeya alipokutana na kamati ya maandalizi ya sherehe
hizo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama pamoja na wajumbe wa kamati
wakiwa katika ukaguzi wa maadalizi ya sherehe za Mei Mosi katika viwanja
vya Sokoine Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na kamati hiyo
wakiangalia mtaro unaopitisha maji katika viwanja vya Sokoine ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya kufikia Kilele cha Sherehe za Wafanyakazi (Mei
Mosi) Jijini Mbeya.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment