Katibu
Tawala Mkoa wa kagera Profesa Faustin Kamuzora akizungumza wakati wa
mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania
na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera, wa pili kushoto ni Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt
Faraja Mnyepe, kushoto ni Balozi Paul Mkumbya kutoka Wizara ya Mambo ya
Nje ya Uganda na kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Paul Makelele.
Ujumbe
wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Mahusiano kujadili changamoto
zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani
Kagera wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe (hayupo pichani) wakati wa
ufunguzi wa mkutano huo wa siku mbili.
Sehemu
ya washiriki wa mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili
nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika
(kulia) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Tanzania wanaoshiriki mkutano
wa mahusiano kujadili changamoto zinazoikabili nchi za Tanzania na
Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu
Wizara ya Mifugo Elisante Ole Gabriel na anayemfuatia ni Katibu Mkuu
Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja
Mnyepe.
Balozi
wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima (Kushoto) akimsikiliza Mpima
Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Julius Msofe (wa
pili kulia) wakati wa mkutano wa mahusiano kujadili changamoto
zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoa wa
Kagera. Kulia ni Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha.
Balozi
wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima (wa tatu Kulia) akizungumza
wakati wa kujadiliana na ujumbe wa Uganda katika mkutano wa mahusiano
kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda
unaofanyika Bukoba mkoani Kagera. Kulia ni Mthamni Mkuu wa Serikali
Evelyne Mugasha. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).
Na Munir Shemweta, WANMM BUKOBA
Makatibu
Wakuu wa Tanzania na Uganda wanakutana mjini Bukoba mkoani Kagera
katika mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi hizo
ikiwemo Uimarishaji Mpaka wa Kimataifa pamoja na Matumizi endelevu ya
rasilimali za Bonde la mto Kagera..
Mkutano
huo wa siku mbili umeanza tarehe 29 April 2019 mjini Bukoba na
kuwakutanisha Makatibu Wakuu wa nchi hizo mbili kutoka Wizara za Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Wizara ya Mifugo, Wizara ya Maji pamoja na Wizara ya Nishati.
Kabla
ya mkutano huo, Wataalamu wa sekta shiriki kutoka Tanzania na Uganda
walikutana na kujadiliana kuhusiana na changamoto zinazozikabili nchi
hizo mbili kwa nia ya kuwasilisha mapendekezo yaliyofikiwa kwa Makatibu
Wakuu wa nchi hizo.
Baadhi
ya Changamoto zinazojadiliwa kwenye mkutano huo, ni pamoja na
Uimarishaji na Uthamini wa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Uganda,
Mpango kabambe wa utunzaji mto Kagera na Matumizi endelevu ya rasilimali
kati ya Tanzania na Uganda katika Bonde la Mto Kagera.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe alisema
mkutano huo ni mfululizo wa mikutano kati ya nchi hizo mbili wenye
lengo la kutatua changamoto zinazozikabili nchi hizo kwa nia ya kuleta
maendeleo.
Alisema,
pamoja na kuwepo changamoto kadhaa lakini Tanzania na Uganda
zinaendelea kufurahia mahusiano mazuri yaliyopo kwa kukutana na
kujadiliana masuala mbalimbali yenye lengo la kuleta manufaa kwa nchi na
watu wake.
Kwa
upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Profesa Faustin Kamuzora
aliuzungumzia mkutano huo kama njia ya kuzifanya nchi husika kufanya
kazi pamoja na kuzidisha ushirikiano wenye nia ya kuleta maendeleo na
kusisitiza kuwa, utekelezaji wa makubaliano yatakayofikiwa unapaswa
kufanywa kwa wakati.
No comments:
Post a Comment