Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na
mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano
Eng. Isack Kamwelwe wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi
mradi wa Ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Mbinga mjini
mpaka Mbamba Bay km 67, sherehe zilizofanyika Mbinga mkoani Ruvuma.
Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Alex
Mubiru akishuhudia
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata
utepe pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika AfDB Dkt. Alex Mubiru wa pili kutoka kushoto , Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Ruvuma Godfrey Zambi watatu kutoka kulia, Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga wapili kutoka kulia, Mwalikishi wa
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Chrisianus Ako wa kwanza kulia.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika AfDB Dkt. Alex Mubiru wa kwanza kulia aliyekaa wakiwa katika
picha ya pamoja na wakandarasi wa ujenzi wa barabara ya Mbinga mjini
mpaka Mbamba Bay km 67, wafanyakazi, wasimamizi pamoja na viongozi
wengine.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa
kwa wafuraha na wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Mbinga
mjini kabla ya kuwahutubia.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi(Albinism ) wanaosoma Shule ya St.
William iliyopo Mbinga mkoani Ruvuma. Rais Dkt. Magufuli amewachangia
watoto hao kiasi cha Shilingi milioni tatu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wanachi pamoja na Wanafunzi wa Shule mbalimbali za eneo la Kigonsera
(hawaonekani pichani) Mbinga mkoani Ruvuma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wanachi wa Liganga wakati akiwa njiani kuelekea Mbinga mkoani
Ruvuma. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment