Katika
jitihada za kutafutia Watanzania nafasi za masomo nje ya nchi, Ubalozi
wa Tanzania nchini Malaysia umefanikiwa kupata ufadhili (scholarships)
kwa wanafunzi 160 katika fani mbalimbali.
Kwa
mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt Ramadhani Dau,
Ufadhili huo ambao umetolewa na Chuo Kikuu cha UNISEL (University of
Selangor) kilichopo Kuala Lumpur una thamani ya USD 1,851,860 sawa na
shs 4,287,084,410 za Tanzania.
Dkt. Dau amesema ufadhili huo wa masomo utahusu fani zifuatazo:
1. Bachelor of Civil Engineering
2. Bachelor of Electrical Engineering
3. Bachelor of Mechanical Engineering
4. Bachelor of Occupational Health and Safety
5. Bachelor of Medical Laboratory
6. Bachelor of Industrial Biotechnology
7. Bachelor of Computer Science
8. Bachelor of Information Technology
Chuo Kikuu cha Selangor ni miongoni mwa vyuo vya Serikali ambacho kilianzishwa mwaka 1999 na kina program za masomo zaidi ya 90 kwenye ngazi mbalimbali kuanzia stashahada hadi shahada ya uzamivu (PhD). Kwa sasa UNISEL ina wanafunzi
13,500
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau akipokea barua rasmi ya ufadhili huo wa masomo kutoka kwa Profesa Dkt. Mohammad Ridhwan Othman wa
Chuo Kikuu cha UNISEL University of Selangor jijini Kuala Lumpur leo
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau akipokea barua
rasmi ya ufadhili huo wa masomo kutoka kwa Profesa Dkt. Mohammad Ridhwan
Othman wa
Chuo Kikuu cha UNISEL University of Selangor jijini Kuala Lumpur leo
Balozi
wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau akiwa katika picha ya
pamoja baada ya kukabidhiwa barua rasmi ya ufadhili huo wa masomo kutoka
kwa Profesa Dkt. Mohammad Ridhwan Othman wa Chuo Kikuu cha UNISEL University of Selangor jijini Kuala Lumpur leo
Balozi
wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau akitembezwa kwenye maeneo
mbalimbali ya chuo baada ya kukabidhiwa barua rasmi ya ufadhili huo wa
masomo kutoka kwa Profesa Dkt. Mohammad Ridhwan Othman wa Chuo Kikuu cha UNISEL University of Selangor jijini Kuala Lumpur leo
Balozi
wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau akitembezwa kwenye
maeneo mbalimbali ya chuo baada ya kukabidhiwa barua rasmi ya ufadhili
huo wa masomo kutoka kwa Profesa Dkt. Mohammad Ridhwan Othman wa Chuo Kikuu cha UNISEL University of Selangor jijini Kuala Lumpur leo
No comments:
Post a Comment