Tanzania na Serikali ya Umoja ya Libya,
zimekubaliana kuingia katika mazungumzo ya kina yenye lengo la kupitia miradi
yote na uwekezaji, iliyokuwa ikifanywa
na Serikali ya Libya hapa nchini kabla ya machafuko nchini humo na pia
kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji ambayo Libya imeonesha nia ya kutaka
kuwekeza chini ya Kamati ya pamoja baina ya nchi hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo jijini Dar es salaam
wakati wa mazungumzo na Kiongozi wa Ujumbe kutoka Libya na kuongeza kuwa baada
ya hali ya Libya kutengemaa na Amani kuongezeka wamekubaliana kuingia katika
uwekezaji.
“Nimemueleza
mgeni wangu kuwa mwaka huu wa 2019 Tanzania tumeutangaza kuwa ni mwaka wa
uwekezaji na yeye ameonesha nia ya nchi yake na makampuni ya Libya kutaka kuja
kuwekeza hapa nchini,tumejadili pia jinsi ya kufufua kamati ya pamoja kati ya
Libya na Tanzania kwakuwa mkutano wa mwisho ulifanyika mwaka 2000 baada ya
Kamati hiyo kukutana sasa tutajadili miradi mbalimbali ambayo Libya
imewekeza,mitaji iliyoiwekeza lakini pia tutaangalia maeneo mapya
wanayopendekeza kuwekeza”
Aidha Profesa Palamagamba John Kabudi amefafanua
kuwa lengo jipya katika sheria za uwekezaji Tazania ni kuhakikishia Nchi
inakuwa na mfumo wa sheria na uwekezaji ambao kila upande unapata tofauti na
mfumo wa zamani ambao wawekezaji walikuwa wakinufaika na nchi inanyonywa.
Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe kutoka Libya
Mhe. Jamal El Barak amesema wamekuja dhumuni la ujumbe wao kwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ni kumjulisha kuwa Serikali ya
Umoja wa Libya iko tayari kufufua na kuendeleza mahusiano ya kidiplomasia baina
ya nchi hizo baada ya hali ya Amani kutengemaa nchini Libya kutokana na
mahusiano ya Tanzania na Libya kuwa ya kihistoria.
Mbali na hayo Mhe Jamal El Barak ameongeza kuwa
Libya iko tayari kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali za uwekezaji
kwa kuwa wanatambaua mazingira ya uwekezaji Tanzania ni mazuri hasa baada ya
kuhakikishiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki
kuwa mazingira ya uwekezaji yameboreshwa.
“Si mara yetu ya kwanza kuwekeza hapa
nchini,kabala ya machafuko nchini mwetu tulikuwa tumewekeza katika sekta
mbalimbali na sasa tutaangalia maeneo mapya ya uwekezaji”
No comments:
Post a Comment