Akizungumzia
kuhusu utoaji wa huduma katika Mji wa Serikali, Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amesema,
ofisi yake iko tayari na imejipanga kikamilifu kutoa huduma kwa wananchi
na wadau wote wa masuala ya kiutumishi na utawala bora.
Dkt.
Ndumbaro ametoa wito kwa wananchi, watumishi wa umma na wadau wengine
kufuata huduma katika ofisi yake iliyopo Mtumba kwenye Mji wa Serikali
na kuongeza kuwa, kwa sasa Idara zilizohamia ni ya Utawala na Utumishi
wa Umma na ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu ambazo zina wateja wengi,
hivyo watumishi wa umma na wananchi wajitokeze kupata huduma.
Aidha,
Dkt. Ndumbaro amesisitiza kuwa, mwananchi au mtumishi yeyote mwenye
uhitaji wa kupata huduma kutoka kwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na
Naibu Katibu Mkuu wafike katika ofisi za Mtumba ili waweze kuhudumiwa
ipasavyo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13
Aprili, 2019, alizindua rasmi ofisi za wizara zilizojengwa katika Mji
wa Serikali na kuelekeza Watumishi waanze kutoa huduma kwa wananchi
mapema iwezekanavyo.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean
Ndumbaro, akizungumza kuhusu ofisi yake kuanza kutoa huduma kwenye Mji
wa Serikali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizindua ofisi za Wizara
zilizojengwa katika mji huo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean
Ndumbaro, akifurahia jambo na wasaidizi wake baada ya ofisi yake kuanza
kutoa huduma kwenye Mji wa Serikali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wakati
akizindua ofisi za Wizara zilizojengwa katika mji huo kwa ajili ya
kutoa huduma kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment