Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji , amewataka Watumishi
wa Wizara hiyo kuendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato ya ndani
na kupanua wigo wa walipakodi pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu wa
mapato kutoka vyanzo mbalimbali.
Dkt.
Kijaji ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza
la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kambarage,
wizarani hapo.
Alisema Wizara ya Fedha na Mipango imebeba majukumu ya kuhakikisha kuwa mapato ya Serikali na matumizi ya rasilimali fedha yanasimamiwa kikamilifu.
“Watendaji
na watumishi wote wa Wizara wanawajibu wa kuimarisha mifumo ya
usimamizi wa fedha na ufuatiliaji wa matumizi ili kuhakikisha rasilimali
fedha zilizopo zinatumika kwa ufanisi” ,alisema Dkt. Kijaji.
Alisema
ni jukumu la Watumishi wa Wizara kugawa rasilimali fedha kwa kuzingatia
vipaumbele vilivyoainishwa kwenye Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo
wa Miaka Mitano (2016-2021) wenye dhima ya kujenga uchumi wa viwanda
ili kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu.
Aliwataka
Watumishi kufanyakazi kwa ushirikiano, umoja , mshikamano, ufanisi na
uadilifu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali
iliyopo.
“Ni
wajibu wetu pia kutumia busara na hekima, hususan pale
tunaposhughulikia maslahi ya watumishi na wananchi kwa ujumla”,
alisisitiza Dkt. Kijaji.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Wafanyakazi, Bw. Doto James, amemhakikishia Dkt. Kijaji kuwa
watatekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa haraka na ukamilifu kwa
maendeleo ya nchi kwa kuwa Wizara hiyo ni nguzo ya kusimamia uchumi wa
nchi.
Alisema
uzoefu unaonesha kwamba vikao vya Baraza la wafanyakazi vimekua na
umuhimu mkubwa mahala pa kazi na kwa kuzingatia umuhimu huo Wizara ya
Fedha na Mipango imehakikisha kuwa vikao vya Baraza vinafanyika kila
mwaka kulingana na Mkataba kati ya Wizara na Chama cha Wafanyakazi cha
Serikali na Afya (TUGHE).
Alisema
kupitia Baraza la wafanyakazi Wizara imefanikiwa kuongeza mshikamano
kati ya Wafanyakazi hivyo kuamsha ari kwa watumishi kufanya kazi kwa
kushirikiana na Viongozi wa Serikali.
Aliongeza
kuwa hoja mbalimbali zilizowasilishwa kwenye Baraza zimeboresha huduma
kwa watumishi, kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ikiwemo kuwapatia
watumishi vitendea kazi pamoja na kuwelimisha watumishi kuhusu magonjwa
sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu (BP), Kifua kikuu, HIV na
UKIMWI.
Meza
Kuu (waliyokaa) ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Ashatu Kijaji (Mb),(watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja
na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo wakati wa ufunguzi wa
Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa
Kambarage, Jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Bw. Doto James akitoa ufafanuzi kwa
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kabla ya
kuanza Baraza la Wafanyakazi wa Wazara hiyo lililofanyika katika ukumbi
wa Kambarage Jijini Dodoma .
Meza
Kuu ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu
Kijaji (Mb), (watatu kushoto) wakiimba wimbo wa kudumisha umoja kabla ya
kuanza Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, Jijini Dodoma .
Wakuu
wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiimba wimbo wa
kudumisha umoja na mshikamano "solidarity forever" kabla ya kuanza
Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma .
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kushoto)
akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo aliyeteuliwa na
Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuapishwa hivi karibuni ,
Bw. Adolf Ndunguru, katika Baraza la Wafanyakazi wa Wazara hiyo ,
Dodoma.
Mwenyekiti
wa Baraza la Wafanyakazi na Katibu Mkuu wa Waziri wa Fedha na Mipango,
Bw.Doto James akitoa salam za utangulizi kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), wakati wa
ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika
ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.
Sehemu
ya Wajumbe walioshiriki Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na
Mipango wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), katika ukumbi wa
Kambarage Dodoma ambapo Watendaji wa Wizara walitakiwa kutekeleza jukumu
la kugawa rasilimali fedha kwa kuzingatia vipaumbele vilivyoainishwa
kwenye Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akizungumza
wakati wa kufungua Baraza la Wafanyakazi, Jijini Dodoma, ambapo aliagiza
Watendaji wa Wizara hiyo kuendelea kuboresha mifumo ya kukusanya mapato
ya ndani ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa walipa kodi.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akipongezwa na
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.Doto James, baada ya
kumaliza hotuba yake alipofungua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo
lililofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment