Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na uzalishaji wa Kilimo cha
Alizeti {Sun Flower} la Alemdar kutoka Nchini Uturuki limeonyesha nia
ya kutaka kujenga kiwanda kitakachozalisha Bidhaa tofauti kwa kutumia
malighafi ya Maua hayo katika azma ya kuitikia wito wa Serikali wa
kuwa Nchi ya Viwanda katika kipindi kifupi kijacho.
Ofisa Mkuu wa Shirika hilo Bibi Fatma Atala alieleza hayo wakati
Ujumbe wa Viongozi wa Shirika hilo ulioongozwa na Mwenyekiti wake
Bwana Oktay Alemder ulipokutana kwa mazungumzo na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Bibi Fatma Atala alisema Mradi huo wa Kibiashara endapo utafanikiwa
kuanzishwa Visiwani Zanzibar unalenga pia kuwashirikisha moja kwa moja
Wakulima Vijini kwa kulima Maua ya Alizeti katika baadhi ya maeneo yao
ya Kilimo.
Alisema Maua ya Alizeti ni bidhaa inayoendelea kuwa na hadhi kubwa
katika masoko ya Kimataifa ambayo inaweza kusaidia kunyanyua mapato ya
washiriki katika ukulima wake sambamba na kuongeza Mapato ya Taifa.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi alueleza Ujumbe huo wa Viongozi wa Shirika la Alemdar kutoka
Nchini Uturuki kwamba Tanzania tayari imeshaamua kuwa Nchi ya Viwanda
ifikapo Mwaka 2025.
Balozi Seif alisema Wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi wana fursa ya
kuitumia nafasi hiyo katika Ushiriki wao wa Uwekezaji utakaokwenda
sambamba na azma hiyo ya Serikali.
Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba
Ujumbe huo unapaswa kuzingatia zaidi mazingira halisi ya Zanzibar
yanayoendelea kukumbwa na changamoto la ufinyu wa Ardhi.
Balozi Seif aliushauri Ujumbe wa Viongozi hao kutayarisha maombi na
kuyawasilisha kwa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA}
kwa hatua ya kuangalia uwezekano wa kuufanyia uchambuzi yakinifu Mradi
wao na mazingira halisi ya Ardhi yaliyopo Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Ujumbe huo wa
Viongozi wa Shirika la Alemdar kwamba Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar iko tayari muda wowote kuunga mkono jitihada za Shirika hilo
za kutaka kuitumia fursa ya Uwekezaji Vitega Uchumi iliyopo Nchini
Tanzania.
Mwenyekiti
wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na uzalishaji wa Kilimo cha
Alizeti (Sun Flower) la Alemdar Bwana Oktay Alemder Kushoto
akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alipofika na Ujumbe wake kwa mazungumzo. Kati kati yao ni Mwakilishi wa
Shirika hilo hapa Zanzibar Bibi Batuli.
Mkuu
wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na uzalishaji wa Kilimo cha
Alizeti (Sun Flower) la Alemdar Bibi Fatma Atala Kushoto akitoa maelezo
ya utendaji wa Shirika lake kwa Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe
wa Viongozi wa Shirika la Alemdar kutoka Nchini Uturuki Afisini kwake
Vuga Mjini Zanzibar.
Baadhi
ya Viongozi wa Shirika la Kimataifa
linalojishughulisha na uzalishaji wa Kilimo cha Alizeti (Sun Flower) la
Alemdar wa Uturuki na wale waliopo Zanzibar wakifuatilia mazungumzo
yao na Balozi Seif hayupo pichani.
Picha na – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment