Waziri
wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi ,William Lukuvi,amezitaka Taasisi
za Kifedha hapa nchini ikiwemo Benki kuwawezesha wananchi wa hali ya
chini kupata mikopo ya nyumba kwa riba nafuu.
Aidha
amezitaka taasisi hizo za kifedha kushirikiana na kampuni za ujenzi ili
kuwasaidia wananchi wanaochukua mikopo kwa ajili ya ujenzi wa
nyumba,kumiliki nyumba kwa gharama nafuu.
Waziri
Lukuvi aliyasema hayo jijini Arusha katika maonyesho ya NMB Nyumba
Day,yaliyofanyika jijini hapa na kukutanisha wateja na watoa huduma
katika ujenzi na uuzaji wa nyumba ambapo Benki ya NMB inatoa huduma ya
mikopo kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kumiliki nyumba.
Amesema
kuwa taasisi za fedha zinazotoa mikopo ya nyumba zinatakiwa kutafuta
namna ya kuwasaidia wananchi ili kuweza kumudu na kupata nyumba kwa
gharama nafuu.
"Ili
gharama za ujenzi wa nyumba za Tanzania zisiwe za ghali taasisi za
kifedha kuweni na mpango mahsusi,endelevu na ulio rahisi wa kumkopesha
mtu nyumba,ili wananchi wa hali ya chini kupata mikopo kwa riba nafuu na
mshirikiane na kampuni za ujenzi ili kuwasaidia wananchi wanaochukua
mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba,kumiliki nyumba kwa gharama nafuu,"
alisema
Waziri
Lukuvi aliipongeza Benki ya NMB kwa kuanzisha mikopo hiyo ambapo ni
miongoni mwa Benki zilizopo hapa nchini ambazo zinashirikiana na wadau
wengine kuhakikisha wananchi wanapata mikopo kwa riba nafuu na
kuwawezesha kumiliki nyumba za makazi.
Awali
Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati kutoka Benki ya NMB,Salie
Mlay,anasema benki hiyo imekuwa baina ya wananchi na serikali katika
kuwawezesha wananchi ili wapate makazi bora.
WAZIRI
wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi ,William Lukuvi,maonesho ya NMB
Nyumba Day,yaliyofanyika jijini Arusha akimsikiliza mmoja wa Wadau wa
Maonesho hayo wakati wa maonesho hayi yaliyowakutanisha wateja na watoa
huduma katika ujenzi na uuzaji wa nyumba ambapo Benki ya NMB inatoa
huduma ya mikopo kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kumiliki
nyumba.Pichani kulia ni Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati kutoka
Benki ya NMB,Salie Mlay.
Waziri
wa Ardhi,Nyumba Maendeleo na Makazi William Lukuvi,akizungumza na
wananchi jijini Arusha leo,katika hafla ya maonyesho ya nne ya NMB
Nyumba Day,yaliyofanyika katika eneo la Baracuda,jijini Arusha,maonyesho
yaliyolenga kuwakutanisha wateja na watoa huduma za ujenzi na uuzaji wa
nyumba ambapo benki ya NMB inatoa huduma ya mikopo kwa ajili ya
kuwawezesha wateja wake kumiliki nyumba
No comments:
Post a Comment