Kazi za Mwenyekiti wa Mtaa/Kijiji.
Ni msemaji Mkuu wa kisiasa na mwakilishi wa Serikali ya Kijiji.
Kuwakilisha kijiji katika vikao au mikutano ya Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC)
Kuitisha na kuongoza mikutano ya halmashauri ya kijiji na
mikutano mikuu ya kijji
7
Kusimamia na kuhamasisha wakazi wa kjiji katika kutekeleza shughuli za maendeleo;
Kuwaongoza na kuwahamasisha wakazi wa kijiji washiriki katika mikutano ya hadhara inayoandaliwa na Serikali au Halmashauri ya Kijiji;
Kuwakilisha maamuzi/maazimio ya vikao vya Kamati ya Maendeleo ya Kata na ya halmashauri ya Wilaya kwenye vikao au mikutano ya kijiji.
Kutunza rejesta ya wakazi wote wa kijiji.
Kusimamia na kuhamasisha ulinzi na usalama wa watu na mali zao.
Kushirikiana na Afisa Mtendaji wa Kijiji kukusanya mapato ya kijiji na halmashauri ya wilaya.
Kushughulikia migogoro midogo midogo isiyostahili kushughulikiwa na mabaraza ya ardhi ya vijiji au kata au mahakama ya mwanzo.
No comments:
Post a Comment