Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt
Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi
wa Umoja wa Ulaya (EU), nchini leo tarehe 1 Mei, 2019, katika ofisi
ndogo za wizara jijini Dar es salaam. Mazungumzo hayo yamejikita katika
kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na EU hususan katika nyanja
za elimu na udhibiti wa biashara haramu ya dawa za kulevya.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt
Damas Ndumbaro (Mb.), akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo.
Kaimu Balozi Stuart akielezea jambo wakati wa mazungumzo hayo.
Afisa
Mambo ya Nje wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Albert Philipo akifuatilia
mazungumzo hayo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt
Damas Ndumbaro (Mb.) akiagana na Kaimu Balozi Charles Stuart mara baada
ya mazungumzo.
No comments:
Post a Comment