Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania
na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, Kiuchumi na
Kimazingira umemalizika Bukoba mkoani Kagera kwa Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe na
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot kusaini
makubaliano yaliyofikiwa.
Mkutano huo wa siku mbili ulimalizika na kuwakutanisha Makatibu
Wakuu wa nchi za Tanzania na Uganda kutoka Wizara zinazoshughulika na
masuala ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mambo ya Nje, Mifugo
na Uvuvi, Maji pamoja na Nishati.
Kabla ya mkutano huo, Wataalamu wa sekta zinazohusika kutoka nchi hizo
mbili walikutana na kujadiliana namna bora ya kukabiliana na
changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda katika eneo la
Mpaka na baadaye kuwasilisha mapendekezo kwa Makatibu Wakuu kwa lengo
la kujadiliwa kwa manufaa ya nchi hizo.
Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja na
Uimarishaji na Uthamini wa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Uganda,
Mpango Kabambe wa Utunzaji Mto Kagera na Matumizi Endelevu ya
Rasilimali za Bonde la Mto Kagera kati ya Tanzania na Uganda.
Akizungumza baada ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel alisema katika siku mbili za
mkutano huo, nchi washiriki zilijadili namna bora ya kuendeleza
mahusiano ya mipakani kwa lengo la kurahisisha mambo ya kiuchumi,
kijamii na kimazingira sambamba na kujadili jinsi ya kuboresha
matumizi endelevu ya Rasilimali za Bonde la Mto Kagera ili ziweze
kuleta manufaa kwa nchi za Tanzania na Uganda.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda
Alfred Okidi Ollot alisema, mkutano huo ni njia sahihi ya kuonesha
kuimarika kwa mahusiano ya Tanzania na Uganda na kusisitiza kuwa
kilichofanyika ni kuonesha uhalisia wa ushirikiano kwa lengo la
kuwafanya wananchi wa pande zote kunufaika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Dkt Faraja Mnyepe alizishukuru pande zote mbili za nchi za
Tanzania na Uganda kwa kufanikisha kufikiwa makubaliano aliyoyaeleza
kuwa yana lengo la kuleta manufaa kwa nchi za Tanzania na Uganda.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.
Faraja Mnyepe (wa tatu kulia) akibadilishana hati za makubaliano na
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot baada ya
kusainiwa kwenye Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa
kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii,
kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera. Wa kwanza
kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.
Faraja Mnyepe (wa tatu kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira
wa Uganda Alfred Ollot wakionesha hati za makubaliano baada ya
kusainiwa kwenye Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa
kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii,
kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera. Wa kwanza
kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.
Faraja Mnyepe (wa tatu kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira
wa Uganda Alfred Ollot (Wa pili kushoto) wakisaini Makubaliano
yaliyofikiwa katika mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa
Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya
kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera. Wa
kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.
Faraja Mnyepe akizungumza wakati wa kuhitimisha Mkutano wa Kuendeleza
Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya
kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira Bukoba mkoani
Kagera. (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Mazingira
wa Uganda Alfred Ollot. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
Balozi
wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima (wa kwanza kulia) na Katibu
Tawala wa mkoa wa Kagera Profesa Faustin Kamuzora wakifuatilia maelezo
yaliyokuwa yakitolewa wakati wa kufungwa Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano
ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya
kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira Bukoba mkoani
Kagera.
Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na Makatibu Wakuu ukifuatilia Mkutano wa
Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda
kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira
uliomalizika Bukoba mkoani Kagera.
Balozi
wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima akizungumza kwenye Mkutano wa
Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda
kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira
uliomalizika Bukoba mkoani Kagera.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya
pamoja na Washiriki wa Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa
Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala
ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani
Kagera (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Mazingira
wa Uganda Alfred Ollot. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa kwanza kulia ni
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
(PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WA WIZARA YA ARDHI)
No comments:
Post a Comment