Mkurugenzi
wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi akitoa taarifa ya utoaji mikopo wakati wa
hafla ya utoaji mikopo kwa vikundi katika Jiji la Dodoma
|
Alisema kuwa halmashauri
zingine zihakikishe kuwa asilimia 10 ya mapato yao ya ndani inapelekwa moja kwa
moja kwenye vikundi vya wanawake na vijana na watu wenye ulemavu ili kuwainua
kiuchumi.
“ Jiji la Dodoma limekuwa la
mfano katika mambo mengi kuanzia ukusanyaji wa mapato wameongoza katika pato
ghafi na leo hii wametekeleza kwa vitendo Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa
Sura Na, 290 kifungu 37A na kanuni zake za utoaji na usimamizi wa mikopo kwa
vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu za mwaka 2019.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo
akiwa na viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Dodoma wakati wa hafla ya utoaji mikopo
kwa vikundi Jijini Dodoma.
|
“Unajua wananchi wetu
wanataka kufanikiwa katika biashara na pia wanapendelea biashara kubwa hivyo
mkibuni mradi mkawatengenezea vizuri kisha mkawakabidhi kama sehemu ya mkopo
itawajenga na kubadilisha maisha yao kuliko kila siku kuwapa fedha ni vyema
wakati mwingine mkawapa vitega uchumi,” aliongeza Jafo.
Naye Mstahiki Meya wa Jiji la
Dodoma Prof. Davis Mwamfupe amesema Jiji la Dodoma pamoja na kutoa mikopo hii
wameenda mbali zaidi kwa kuhakikisha wanatafuta vyuo vya kutoa ujuzi na maarifa
zaidi kwa wanufaika wa Mikopo ili iweze kuwa na tija zaidi.
Pia alisema katika siku
zijazo wanatarajia kutoa vifaa na vitendea kazi vya biashara zao kuliko kuwapa
fedha ili kuwaepusha na vishawishi vinavyoweza kutokea kutokana na kushika fedha
mkononi.
Naye Mkurugenzi wa Jiji hilo,
Godwin Kunambi alisema kuwa Jiji la Dodoma limeanza kutoa mikopo kwa vikundi kuanzia
mwaka wa fedha wa 2015/16 hadi Desemba 2018 ambapo jumla ya shilingi 2,434,757,316
ziko kwenye mzunguko wa mikopo ya vikundi.
Aliongeza kuwa kiasi cha
zaidi ya Sh bilioni 2.6 (2,606,645,760) zilitengwa kwenye bajeti ya mwaka wa
fedha 2018/19 huku kiasi cha shilingi 1,796,730,000 kimeshatolea katika kipindi
cha mwezi Julai hadi Disemba 2018.
“Fedha za vikundi
unazokabidhi leo kiasi cha shilingi 1,062,500,000 zinaifanya Halmashauri ya
Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2018/19 kutoa mikopo ya jumla ya shilingi
2,859,230,000 sawa na asilimia 109.6 ya malengo tuliyojiwekea” alisema Kunambi.
Jumla ya vikundi vya
wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vilivyokwishanufaika na mikopo ya
Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuanzia mwaka 2015/16 mpaka sasa ni 1,020 vyenye
jumla ya Wanachama 10,200 vikiwa na mzunguko wa jumla ya shilingi
3,497,257,316.
Nteghenjwa
Hosseah, OR-TAMISEMI
No comments:
Post a Comment