Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Janeth
Magufuli, amewasihi Waislamu nchini kuendelea kuliombea Taifa muda
wote, hususan katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani, na kuendeleza mshikamano bila kujali dini ama kabila tabaka
zao.
Mama Magufuli ametoa wito huo leo tarehe 22 Mei, 2019 Jijini Dar es
Salaam wakati akitoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi
mbalimbali vyenye uhitaji.
Vyakula alivyotoa ni tani 5 za mchele, tani 3 za sukari na tende.
Hafla hiyoimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Mruma,
Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile na wawakilishi
wa vikundi mbali mbali vya wenye uhitaji.
Mama Magufuli pia amemuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema,
azikubali funga za Waislamu wote na kuwalipa malipo stahiki wakati
wakitekeleza moja ya nguzo muhimu za Dini ya Kiislamu.
“Kipindu cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kipindi cha toba. Ni
kipindi cha kutenda matendo mema na kujizuia na vitendo viovu” amesema
Mama Magufuli.
Mama Magufuli amesema licha ya kwamba Tanzania ina watu wa imani za
Dini tofauti lakini siku zote wananchi wake wamekuwa wakishirikiana
nyakati za dhiki na za raha bila ubaguzi.
Ametoa mfano kuwa licha ya tofauti za kidini zipo baadhi ya familia
ambazo Baba Muislamu na Mama ni Mkristo zinaishi kwa amani na
kus
hirikiana katika masuala yote ya kifamilia na kwamba sifa hii ni
moja nguzo muhimu za umoja wa Watanzania.
“Binafsi nakumbuka zamani nikiwa mdogo tulikuwa tunatafuta Mwislamu
aje atuchinjie kuku ama mbuzi ama ng’ombe” , alisema na kuongezea: “Ni
kutokana na utamaduni huo uliojengeka miongoni mwa Watanzania , leo
nimeguswa kutoa sadaka yangu kwa ajili ya ndugu zangu wenye uhitaji…”
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli,
akiongea machache wakati wa hafla ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili
ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo
Jumatano Mei 22, 2019.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli,
akimsiliza Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Muma akitoa shukurani
wakati wa kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi
mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22,
2019.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli,
akimkabidhi Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Muma msaada wa vyakula
kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji
jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 019
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli,
akimkabidhi Mkurugenzi wa Hija wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile msaada
wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye
uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli katika
picha ya kumbukumbu na Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Mruma,
Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile pamoja na
wawakilishi wa vikundi mbali mbali vya wenye uhitaji baada ya hafla ya
kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali
vyenye uhitaji.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama
Janeth Magufuli, akimkabidhi mmoja wa wawakilishi msaada wa vyakula
kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji
jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
No comments:
Post a Comment