Rais
Dkt.John Magufuli siku 30 Ofisi ya Rais-IKULU, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi
ya Waziri Mkuu, Wizara pamoja na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma,kutum
kutumia huduma za Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Nchini (TTCL)ikiwemo laini,
ili kupanua huduma za mawasiliano ya Mtandao wa Kampuni hiyo nchini.
Akizungumza wakati wa
Hafla ya kukabidhi gawio kwa Serikali la Tsh Bilioni 2.1 kutoka TTCL, Rais
Magufuli alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa TTCL kumuorodheshea nam,ba za simu za
Viongozi na Watendaji wote wa Serikali ikiwemo Mawaziri na Makatibu Wakuu kuona
kama wanatumia laini za simu za TTCL.
Aliongeza kuwa tangu
atoe agizo lake mwaka jana, kuhusu matumizi ya huduma za mawasiliano ya TTCL
katika Ofisi mbalimbali za Umma, hakuna Ofisi yoyote ilitekeleza agizo hilo
ukiondoa baadhi ya Taasisi chache ikiwemo Jeshi la Wananchi Tanzania na Jeshi
la Polisi Nchini.
“Nimefurahi alipokuwa
akitaja Taasisi na Mashirika ambayo yamejiunga moja kwa moja na kutumia huduma
za TTCL, nilisikitika sana niliposikia Ofisi yangu haikutajwa, pia Ofisi ya
Chama changu cha mapinduzi, sasa kama wamesikia na wako hapa nataka kipindi cha
mwezi mmoja tuanze kutumia simu za TTCL”, Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli
alizitaka Ofisi zingine za Serikali kutumia huduma za Kampuni ya Mawasiliano
Nchini ili kuinua na kuimarisha utendaji kazi wake katika nyanja mbalimbali za
maendeleo nchini na kuzitaka Taasisi zingine ziige huo kwa vitendo na siyo
maneno.
“Si Ofisi ya Makamu wa
Rais, Si Ofisi ya Waziri Mkuu, Si Ofisi ya Rais, Si Wizara ya Fedha, hata
Wizara yako ya Mawasiliano na Uchukuzi nayo haijatajwa hapa, nataka kusema
tusipounga Mkono, vyetu tutachezewa mno, tusipowaimarisha hawa TTCL, hawatafika
mbali, lakini wakipata ushirikiano matokeo tutayaona”, Rais Magufuli.
Rais Magufuli alieleza
kuwa kabla ya Shirika hilo halijarudishwa Serikalini, katika kipindi cha miaka
15 kutoka mwaka 2001 TTCL ilikuwa ikipata hasara ya Tsh Bilioni 15 kila mwaka,
huku likishindwa kutoa gawio lolote kwa Serikali.
“Wakati Shirika hili
likiendeshwa na Wabia wetu, lilikuwa halitoi gawio lolote, lakini pia lilikuwa
likipata hasara ya Bilioni 15 kwa mwaka, kwa hiyo mnaweza mkaelewa hii ina maana
gani kwenye uchumi wa nchi, hivyo basi kuweza kufikia hatua hii ya kupata faida
ya Tsh.bilioni 8.3, na kuweza kutoa gawio la Serikali Tsh.bilioni 2.2 ni
mafanikio makubwa’ alisema Rais Dkt Magufuli.
Pia Rais Magufuli alisema
kuwa Sekta ya Mawasiliano kwa sasa imepanuka
nchini na kuwezesha sekta nyingine kufanya kazi kwa ufanisi kwani katika
sekta mbalimbali kwa sasa sekta hii inahitajika sana.
“Sekta ya Mawasiliano
imesaidia kukua kwa sekta nyingine kama sekta ya fedha, ambapo mwaka jana
miamala ya fedha ilifanyika kwa njia ya kimtandao ilikuwa na thamani ya Tsh Trilioni
139.2 sawa na Trilioni 11.6 kwa mwezi, lakini pia sekta ya mawasiliani ni
kichocheo kikubwa kwa Sekta za Elimu, Afya, Biashara, Kilimo, Viwanda Ufugaji, Utalii na Ujenzi”, Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment