Shirika la AGPAHI (Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative) linalojishughulisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi nchini Tanzania, limetoa huduma ya upimaji afya bure kwa wananchi mkoani Simiyu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani 2019 ambayo kilele chake ni Mei 05 kila mwaka.
Huduma hiyo imetolewa katika uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi yalikofanyika maadhimisho hayo ambapo wananchi hususani akina mama walipata fursa ya kufanya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi pamoja na VVU kuanzia Mei 02, 2019.
Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Simiyu, Dafrosa Shiluka akizungumza na BMG kwenye maadhimisho hayo.
Akitoa
takwimu za awali jana kabla hatujaenda mitamboni, Mratibu wa Shirika la
AGPAHI mkoani Simiyu, Dafrosa Shiluka alisema zaidi ya akina mama 200
walifanyiwa uchunguzi na kati hao, mmoja aligundulika kuwa na dalili za
awali za Saratani ya Mlango wa Kizazi na kuanzishiwa huduma ya mgandisho
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Simiyu, Somanda huku wengine wawili
wakipewa rufaa.
Pendo Mboje ambaye ni Mkazi wa Bariadi akizungumza na BMG kuhusu huduma ya upimaji iliyotolewa na Shirika la AGPAHI.
“Lakini
pia akina mama wawili walikutwa na Saratani ya Mlango wa Kizazi ambapo
tuliwapa rufaa ya kwenda Bugando (Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa)
kwa ajili ya matibabu zaidi” alieleza Shiluka.
Mkuu wa Wilaya Busega, Festo Kiswaga akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani 2019 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka.
Shiluka
pia aliongeza kwamba akina mama 166 walikubali kupima maambukizi ya VVU
ambapo kati yao, mmoja alikundulika kuwa na maambukizi ya VVU na
kuanzishiwa dawa kupitia Kituo cha Afya Muungano.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
“AGPAHI
tunatoa huduma za tiba na matunzo kwa wanaoishi na maambukizi ya VVU
katika Wilaya zote za Mkoa Simiyu ambapo tuna jumla ya Vituo 73 ambavyo
tunavihudumia kwa ajili ya huduma hiyo na Vituo vinane kati ya 73
vinatoa huduma ya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi” alisema
Shiluka.
Washiriki wa Siku ya Wakunga Duniani 2019 yaliyofanyika kitaifa Bariaadi mkoani Simiyu wakiwasili uwanjani.
Shiluka
alitoa rai kwa wananchi hususani akina mama kuwa na desturi ya
kujitokeza kupima saratani ya mlango wa kizazi kwenye Vituo vya Afya na
Hospitali zinazotoa huduma hiyo tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi
hujitokeza tu kwenye makongamano mbalimbali mkoani Simiyu.
Viongozi mbalimbali kwenye maadhimisho hayo akiwemo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile (wa tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya Busega Festo Kiswaga (wa pili kulia), Rais wa TAMA Feddy Mwanza (wa tatu kulia), Makamu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Hashina Begum (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Simiyu (wa kwanza kushoto).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akisikiliza ufafanuzi alipotembelea banda la Shirika la AGPAHI.
Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Simiyu, Dafrosa Shiluka (kushoto) akitoa ufafanuzi wa huduma zinazotolewa na Shirika hilo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile (kulia).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akipokea kipeperusha chenye elimu kuhusu Saratani ya Mlango wa Kizazi alipotembelea banda la Shirika la AGPAHI.
Sehemu ya akina mama waliojitokeza kupata huduma ya uchunguzi kwenye banda la Shirika la AGPAHI.
Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Simiyu, Dafrosa Shiluka akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wananchi waliofika kwenye banda la Shirika hilo.
Sehemu ya akina mama waliojitokeza kupata huduma ya uchunguzi kwenye banda la Shirika la AGPAHI.
Baadhi ya Wakunga waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani 2019 kitaifa mjini Bariadi.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments:
Post a Comment