Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Serikali ya Denmark kupitia
ubalozi wake nchini wamesaini mkataba wa makubaliano wa kifedha katika
mwendelezo wa kusaidia maboresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni
pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na
upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini makubaliano hayo balozi wa Denmark nchini Mheshimiwa Einar Hebogard Jensen amesema kuwa mkataba huo umeelekezwa katika sekta tatu ambazo ni programu za utawala bora, upatikanaji wa haki na haki za binadamu.
Katika makubaliano hayo Serikali ya Denmark imetoa msaada wa Krona milioni 7 sawa na takribani dola za kimarekani milioni 1, 049, 776 huku tafiti zikionesha kuwa kwa mwaka 2018 walitoa jumla ya dola za kimarekani milioni 63.
Balozi Jensen amesema kuwa Denmark inaamini kuwa ili kufikia maendeleo lazima misingi ya uwazi, uwajibikaji na usawa wa kijinsia iwepo na wamekuwa na ushirikiano duniani kote na kupitia UNDP nchini Tanzania wamekuwa wakishiriki na kufanya kazi kwa pamoja katika kuboresha shughuli za bunge, utawala bora pamoja na taasisi na vituo mbalimbali za haki za binadamu.
Aidha amesema kuwa watanzania wanazijua haki zao kwa kufuata sheria na hiyo ni kutokana na ukomavu wa demokrasia nchini.
Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Natalie Boulcy amesema kuwa Denmark ni moja kati ya nchi 10 zinazoshirikiana na kutoa msaada mkubwa kwaUNDP hasa katika masuala ya haki za binadamu, utawala bora na ulinzi.
Natalie amesema kuwa msaada utawafikia watu wengi zaidi hasa vijijini pamoja na kusaidia sekta mbalimbali zikiwemo tume ya haki za binadamu na utawala bora (CHRAGG) hasa katika kuwajengea uwezo, ikiwa ni pamoja na kuwezesha uchapishaji wa ripoti za haki za binadamu kwa kila mwaka na kuzimbaza kote nchini kwa kushirikiana na Wizara ya Sheria na katiba na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali .
Pia msaada huo utaelekezwa katika makundi mbalimbali wakiwemo wanawake na watoto, ofisi ya Mwendesha Mashtaka mkuu wa serikali (DPP) kupitia Wizara ya sheria pamoja na vituo vya haki za binadamu na utawala bora.

Balozi
wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen (kushoto) pamoja na Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Natalie Bovely
wakikabidhiana mkataba wa makubaliano wa kifedha kwa ajili ya
mwendelezo wa kusaidia maboresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni
pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na
upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu.
Balozi
wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen (kushoto) pamoja na Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Natalie Bovely
wakisaini mkataba wa makubaliano wa kifedha kwa ajili ya mwendelezo wa
kusaidmkatabaresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na
utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na
upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu yaliyofanyika katika
Ubalozi wa Denmark jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Denmark
nchini Tanzania, Einar Jensen.
Balozi
wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen(kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kusaini mkataba wa
makubaliano wa kifedha kwa ajili ya mwendelezo wa kusaidia maboresho ya
sekta za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na utawala bora na ulinzi
kupitia programu ya msaada wa sheria na upatikanaji wa haki. Mpango huo
ni wa miaka mitatu yaliyofanyika katika Ubalozi wa Denmark jijini Dar es
Salaam. Kulia ni mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa UNDP, Natalie Bovely .
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Natalie
Bovel(kulia) akimpa zawadi Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar
Jensen mara baada ya kumaliza kusaini mkataba wa makubaliano wa kifedha
kwa ajili ya mwendelezo wa kusaidia maboresho ya sekta za haki za
binadamu, ikiwa ni pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya
msaada wa sheria na upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu
yaliyofanyika katika Ubalozi wa Denmark jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment