Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akizindua Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama
wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania jijini Dodoma tarehe 3 Mei 2019. Kushoto ni Mwakilishi wa kutoka Taasisi ya Prindex
David Ameyaw na wa pili kulia ni Mtakwimu Mkuu Serikali Dkt Albina
Chuwa.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa taasisi wakati wa
uzindua Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama wa
Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania jijini Dodoma tarehe
3 Mei 2019. Wa pili kushoto waliokaa ni Mwakilishi wa kutoka Taasisi ya
Prindex David Ameyaw na wa pili kulia waliokaa ni Mtakwimu Mkuu
Serikali Dkt Albina Chuwa.(PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
Na Munir Shemweta, DODOMA
Tanzania imeshika nafasi ya nne kati ya nchi tisa
za Kusini na Mashariki mwa Afrika zilizofanyiwa utafiti kwa kuwa na asilimia 64
ya watu wanaoamini kuwa hali ya umiliki wa ardhi na makazi ni salama.
Hayo yalibainika wakati wa
uzinduzi wa Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama wa
Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya
Takwimu, uzinduzi ulifanyika jijini Dodoma.
Akizungumza wakati wa kuzindua Ripoti hiyo, Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema
kiwango hicho ni kikubwa zaidi ya wastani wa asilimia 61 kwa nchi tisa
zilizofanyiwa utafiti katika Afrika ya Magharibi.
Aidha, Utafiti wa Ripoti hiyo unaonesha Tanzania imeshika nafasi ya kumi kati
ya nchi 33 zilizoshiriki katika Utafiti huo kwa kuwa na asilimia zaidi ya
hamsini ya watu wanaomiliki makazi yao wenyewe.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
alisema, matokeo ya utafiti huo yametokana na hatua mbalimbali ambazo serikali
imeendelea kuzichukua ili kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na usalama wa
umiliki wa ardhi na makazi.
No comments:
Post a Comment