Mkurugenzi
wa Utawala na Fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni
nchini(Brella) Bakari Mketo wakati akizungumza na wadau wa biashara
Jijini Tanga waliohudhuria mafunzo ya namna ya urasimishaji kuwapa uwezo
wajasriamali ili waweze kujua namna ya kusajili na kuongeza thamani ya
bidhaa.
Afisa
kutoka Kitengo cha Ubunifu wa Wakala wa Biashara na Leseni (BRELLA)
ambaye pia ni Mkufunzi wa Mafunzo kwa Kanda ya Kaskazini anayefundisha
namna ya mfumo unavyofanya kazi Suzana Senso akizungumza wakati wa
mafunzo hayo ambapo alisema zoezi la uelimishaji limeanza kutoka mwaka
jana desemba walianzia Nyanda za Juu, kanda ya Ziwa,Kanda ya Magharibi
na Kanda ya Kati na sasa wapo kanda ya Kaskazini.
Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia matukio mbalimbali
Mwamko
wa watanzania kusajili biashara zao kupitia Wakala wa Usajili wa
Biashara na Leseni nchini (BRELLA) umeongezeka kutoka makampuni 62 kwa
mwezi hadi kufikia 700 hali inayosababisha na kuwepo kwa mfumo rafiki wa
kuweza kuwafikia kupitia mtandao ambao umekuwa mkombozi kwao.
Hayo
yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Brella Bakari Mketo
wakati akizungumza na wadau wa biashara Jijini Tanga waliohudhuria
mafunzo ya namna ya urasimishaji kuwapa uwezo wajasriamali ili waweze
kujua namna ya kusajili na kuongeza thamani ya bidhaa.
Alisema
hatua hiyo ni mzuri kwa sababu inaonyeshwa namna watanzania hususani
wafanyabiashara walivyokuwa mstari kujisajili kupitia wakala huu na
kuweza kutambulika ambapo alisema idadi hiyo ilitokea makampuni hayo 62
kwenda 200 na baadae sasa kufikia 700 huku wakiweka mipango ya
kuhakikisha wanazidi kuongeza wigo mpaka ili kuongeza idadi ya makampuni
yatakayojisajili
“Baada
ya mfumo wa kutoka kwa vitambulisho vya Taifa na kutakiwa kutumia namba
ya vitambulisho idadi ya makampuni yanayosajiliwa umeongezeka na
kufikia idadi hiyo lakini bado tutaendelea kukutana na wadau kwa kutoa
elimu kuweza kuongeza wigo mpaka “Alisema.
Aidha
alisema malengo yao ni kuhakikisha wanapanua wigo mpaka na kufikia idadi
ya watu 1000 kwa mwezi ili kumhakikisha kila mdau wao anafikia na
huduma yao kwa wakati hali itakayopelekea kumpunguzia mzigo mzito
mwananchi na hivyo pia kuondoa gharama za kufuata huduma hiyo.
‘Usajili
kabla ya mfumo ulikuwa ni mkubwa sana lakini ulikuwa unawagharmi wateja
wetu kutokana na kwamba wengi walikuwa wakiibiwa na vishoka kwa sababu
wanasafiri kutoka Tanga kwenda Dar kutokana na kwamba hapo awali
kutokuwa na matawi na hivyo kupelekea kuingia gharama na kuwapelekea
mzigo mkubwa hivyo kwa kuliona hilo tukatambulisha mfumo huo wa kusajili
kupitia online na mwamko kabla ya mfumo na baada ya mfumo mwamko
umekuwa mkubwa sana”Alisema
Awali
akizungumza wakati wa mafunzo hayo kutoka Kitengo cha Ubunifu wa Wakala
wa Biashara na Leseni (BRELLA) ambaye pia ni Mkufunzi wa Mafunzo kwa
Kanda ya Kaskazini anayefundisha namna ya mfumo unavyofanya kazi Suzana
Senso alisema zoezi la uelimishaji limeanza kutoka mwaka jana desemba
walianzia Nyanda za Juu, kanda ya Ziwa,Kanda ya Magharibi na Kanda ya
Kati na sasa wapo kanda ya Kaskazini.
Alisema
kwenye maeneo ambayo tayari wamepita mwamko umekuwa mkubwa sana
kutokana na wafanyabiashara kueleza namna ya mfumo huo unavyofanya kazi
ikiwemo kukutana na maafisa biashara hivyo kuwa chachu ya ongezeko la
usajili na uelewa umeongezeka sana.
Hata
hivyo alisema baada ya kutoka mkoani Tanga wataekelea kwenye mikoa ya
Kanda ya kaskazini mingine ikiwemo Kilimanjaro,Arusha na Manyara huku
akitoa wito kwa watu watakaosikia wakala huo wapo kwenye mikoa yao
watumie fursa hiyo kupata darasa ambalo litawapa uelewa mkubwa.
No comments:
Post a Comment