Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule Kuu ya Biashara (UBDS) kupitia
Kituo cha Ubunifu na Ujasiriamali cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDIEC) kwa kushirikiana na ufadhili wa European Investment Bank (EIB)
kimetoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo na wakati juu ya ufahamu
kwenye biashara na mipango kabla ya kuanza biashara.
Miongoni mwa masuala waliyofundishwa ni pamoja na kujua mipango ya
kibiashara, vyanzo vya fedha, kujua masoko, namna ya kuwa na bidhaa
bora na jinsi ya kuuza kwa faida pamoja na kufundishwa namna bora ya
kuandaa maandiko ya kibiashara.
Mafunzo hayo ya siku tatu yalianza tarehe 13 na kumalizika Tarehe 15
Mei 2019 yameshirikisha wajasiriamali kutoka ndani na nje ya Dar es
Salaam ili kuweza kutoa nafasi na wigo mpana kwa wajasirimali
kujikumbusha mbinu na namna bopra za kuboresha baishara zao.
Wajasiriamali
wadogo na wakati wakifuatilia maelekezo kutoka kwa mwezeshaji (hayupo
pichani) wakati wa mafunzo ya namna ya kuboresha biashara zao pamoja na
kufahamu mbinu za kujua masoko, bidhaa na namna ya kuuza na kupata
faida. Mafunzo hayo yametolewa na Kituo cha Ubunifu na Ujasiriamali cha
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDIEC) kwa kushirikiana na ufadhili wa
European Investment Bank (EIB) katika jengo la Shule kuu ya Biashara
kuanzia tarehe 13 hadi 15 Mei, 2019.
Wajasiriamali
wadogo na Wakati wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Ujasiriamali
yaliyoendeshwa na Kituo cha Ubunifu na Ujasiriamali cha Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDIEC) kwa kushirikiana na ufadhili wa European
Investment Bank (EIB) katika Jengo la Shule kuu ya Biashara chuo kikuu
cha Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Mteja kutoka Benki ya Access Alexander
akiwaeleza wajasiriamali wadogo na wakati huduma zinazotolewa na benki
ya Access, na namna bora ya kutunza fedha katika akaunti tofauti
zilizopo katika benki hiyo pamoja na kuwafundisha mbinu za kuwekeza na
kukuza mitaji ili waweze kukopesheka kwa urahisi.
No comments:
Post a Comment