Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimfafanulia jambo Mkurugenzi
wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Tumbaku Tanzania na Kiwanda cha
Kusindika Tumbaku (TTPL), Richard Sinamtwa (kulia), wakati Waziri huyo
alipofika Kiwandani hapo mjini Morogoro, kwa ajili ya kusikiliza
malalamiko ya Viongozi Wakuu wa Kampuni hiyo ambao wanadaiwa kufanyiwa
vurugu na Polisi wane waliofika ofisini hapo kwa lengo la kuwakamata kwa
nguvu bila kufuata utaratibu. Kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Morogoro, Mugabo Wekwe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akimsikiliza
Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Tumbaku Tanzania na
Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Richard Sinamtwa, wakati alipokua
anatoa malalamiko yake akidai Polisi Mkoani Morogoro kuingia ndani
Kiwanda chake na kufanya vurugu kwa kulazimisha kuwakamata kwa nguvu
bila kufuata utaratibu viongozi wa Kampuni hiyo. Kushoto ni Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mugabo Wekwe. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza
Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Tumbaku Tanzania na
Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Richard Sinamtwa, alipokua
anashirikiana na Mkurugenzi mwenzake wa Kampuni hiyo, kutoa malalamiko
yao kwa Waziri huyo kuhusu Polisi Mjini Morogoro kuingia ndani Kiwanda
chao na kufanya vurugu kwa kulazimisha kuwakamata kwa nguvu bila kuwa na
kosa lolote. Kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mugabo
Wekwe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment