Matokeo chanyA+ online




Friday, June 28, 2019

RAIS DK. MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WABUNGE WA SADC NA SPIKA JOB NDUGAI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


s%2B%25281%2529
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo Mhe. Boemo Skgoma ambao wameongozana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro alipokutana na kufanya mazungumzo na wageni hao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2019.
s%2B%25282%2529
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya picha ya Tingatinga na Kinyago Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, alipokutana na na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2019.
s%2B%252803%2529
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya picha ya kuchora toka Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, huku akishuhudiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro alipokutana na kufanya mazungumzo na mgeni huyo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2019
s%2B%25284%2529

s%2B%25285%2529
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo Mhe. Boemo Skgoma pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2019
s%2B%25286%2529
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na mgeni huyo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2019 PICHA NA IKULU

WAJUMBE KAMATI TENDAJI MABUNGE JUMUIYA YA MADOLA TAWI LA TANZANIA WAPATIWA SEMINA YA KUJENGEWA UWEZO BUNGENI JIJINI DODOMA

V25A9676
 Mjumbe wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika tawi la Tanzania, Mhe. Dkt. Sware Semesi (kulia) akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo (hawapo kwenye picha) wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika tawi la Tanzania iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Mussa Azzan Zungu
V25A9687
V25A9719
 Mwenyekiti wa Bunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Mussa Azzan Zungu akifungua semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika tawi la Tanzania iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
V25A9802
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dkt. Emmanuel Mallya akiwasilisha maada wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika tawi la Tanzania iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
V25A9856
 Mjumbe wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika tawi la Tanzania, Mhe. Zainab Vullu akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika tawi la Tanzania iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kulia ni Mjumbe wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika tawi la Tanzania, Mhe. Mohamed Mchengerwa
V25A9901
Wajumbe wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika tawi la Tanzania, Sekretarieti ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika tawi la Tanzania pamoja na wawezeshaji wakiwa katika picha ya pamoja baada ya semina ya kujengewa uwezo iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Thursday, June 27, 2019

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA MAADILI NA USALAMA PAMOJA NA KAMATI KUU LUMUMBA

2
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Maadili na Usalama cha chama kilichofanyika katika ofisi ndogo za Makao makuu ya Chama hicho Lumumba Jijini Dar es salaam. June 26, 2019.
3
4
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi kilichofanyika katika ofisi ndogo za Makao makuu ya Chama hicho Lumumba Jijini Dar es salaam. June 26, 2019.
5
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt Ali Mohammed Shein mara baada ya kikao cha Maadili na Usalama pamoja na kikao cha Kamati kuu ya Chama hicho  vilivyofanyika katika ofisi ndogo za Makao makuu ya Chama hicho Lumumba Jijini Dar es salaam. June 26, 2019.
PICHA NA IKULU

Monday, June 24, 2019

PROF. KABUDI AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA


 Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na ujumbe wake akiwa kwenye mkutano pamoja na mwenyeji wake ambaye ni Waziri wa mambo ya nje wa China na na Mjumbe wa Baraza la Taifa Mhe. Wang Yi na ujumbe wake. Mkutano huo umefanyika Beijing,China. June 24, 2019.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiteta na mwenyeji wake ambaye ni Waziri wa mambo ya nje wa China na na Mjumbe wa Baraza la Taifa Mhe. Wang Yi na ujumbe wake mara baada ya kumaliza mkutano baina yao. Mkutano huo umefanyika Beijing,China. June 24, 2019.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi  (Mb) akisaini mkataba wa msaada wa shilingi bilioni sitini bila ya masharti yeyote pembeni yake ni Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la China Bw. Zhou Liujun,akisaini kwa niaba ya serikali ya China. Zoezi hilo limefanyika Beijing,China. June 24, 2019.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi  (Mb) akibadilishana nyaraka na Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la China Bw. Zhou Liujun, mara baada ya kusaini nyaraka hizo. Zoezi hilo limefanyika Beijing, China. June 24, 2019.


Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi  (Mb) akiwa katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 53 za Afrika na taasisi za fedha za China.
 Sehemu ya mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na wajumbe wao waliohudhuria katika wamkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 53 za Afrika na taasisi za fedha za China. Beijing,China. June 24, 2019.

Sunday, June 23, 2019

RAIS DKT MAGUFULI AHANI MSIBA FAMILIA YA ABBAS TARIMBA JIJINI DAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mtendani wa SportPesa Bw. Abbas Tarimba Abbas alipofika kuhani msiba nyumbani kwake Kinondoni Hananasifu jijini Dar es salaam ambapo hivi karibuni wamefiwa na watoto wao wawili (mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki iliyopita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Abbas Tarimba Abbas nyumbani kwake Kinondoni ambaye hivi karibuni amefiwa na watoto wake wawili (mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki iliyopita jijini Dar es
salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisalimiana na mke wa Bw. Abbas Tarimba Abbas nyumbani kwao Kinondoni ambao hivi karibuni wamefiwa na watoto wao wawili (mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki iliyopita jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza na Bw. Abbas Tarimba Abbas nyumbani kwake Kinondoni alipokwenda kuhani msiba ambapo hivi karibuni amefiwa na watoto wake wawili (mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki
iliyopita jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akimpa mkono wa pole Bw. Abbas Tarimba Abbas nyumbani kwake Kinondoni alipokwenda kuhani msiba ambapo hivi karibuni amefiwa na watoto wake wawili (mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki iliyopita jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiagana na Bw. Abbas Tarimba Abbas nyumbani kwake Kinondoni alipokwenda kuhani msiba ambapo hivi karibuni amefiwa na watoto wake wawili (mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki iliyopita jijini Dar es salaam

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA MKONO WA POLE KWA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR KWA KUFIWA NA MKE WAKE JIJINI DAR


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) Mikocheni jijini Dar es salaam ambaye amefiwa na mkewe Dkt. Badria Abubaker Gunar aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiomba dua maalumu na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) pamoja na familia yake nyumbani kwao Mikocheni jijini Dar es salaam kumuombea marehemu Dkt. Badria Abubaker Gunar(Mke wa Naibu katibu mkuu CCM Znz) aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu wa Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa pili wa Rais wa Znz Balozi Sefu Ali Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi  na Viongozi mbalimbali wa  Serikali na Chama cha Mapinduzi wakimuombea dua marehemu Dkt. Badria Abubaker Gunar Mke wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akimsikiliza Gavana wa Benki Kuu Profesa Frolence Luoga akizungumza mara baada ya dua maalumu ya kumuombea marehemu Dkt. Badria Abubaker Gunar Mke wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) ambaye pia alikuwa ni mtumishi wa Benki Kuu (BOT) ,aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiwa msibani wakati wa dua maalumu ya kumuombea marehemu Dkt. Badria Abubaker Gunar Mke wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) ambaye pia alikuwa ni mtumishi wa Benki Kuu (BOT) ,aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiagana na mdau wa Michezo Mzee Kilomoni  pamoja na waombolezaji wengine mara baada ya dua maalumu ya kumuombea marehemu Dkt. Badria Abubaker Gunar Mke wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) ambaye pia alikuwa ni mtumishi wa Benki Kuu (BOT) ,aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiagana na  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dkt. Abdallah Sadala (Mabodi) mara baada ya kumpa pole kufuatia kifo cha  mkewe Dkt. Badria Abubaker Gunar Mikocheni Jijini Dar es salaam, aliyefariki dunia June 22, 2019 jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI MISA TAKATIFU YA MAADHIMISHO YA SHEREHE EKARISTI TAKATIFU KANISA LA MTAKATIFU PETRO JIJINI DAR ES SALAAM



  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki katika Misa ya Maadhimisho ya Sherehe ya Ekaristi Takatifu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili Juni 23, 2019 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Padre Dkt. Alister Makubi, Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam baada ya kushiriki Misa ya Maadhimisho ya Sherehe ya Ekaristi Takatifu kanisani hapo katika  Jumapili Juni 23, 2019. Katikati ni Paroko Msaidizi wa kanisa hilo Padre Paul Haule na Mzee wa Kanisa Dkt. Aldehem Meru

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU WANAOSHITAKIANA MABARAZA YA ARDHI KUGHARIMIA USAFIRI


Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya na kulia kwa Naibu Waziri ni Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini Stela Tulo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Ulanga Mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini Stela Tulo. 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya na wa kwanza kulia ni Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini Stela Tulo. (PICHA ZOTE NA HASSAN MABUYE- WIZARA YA ARDHI) 



Na Munir Shemweta, WANMM ULANGA 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amepiga marufuku wananchi wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi kutoa pesa kwa ajili ya kugharimia usafiri wa kwenda eneo lenye mgogoro. 

Akizungumza wakati wa kuzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki Dkt Mabula alisema, kutoa pesa ya kugharamia usafiri kwa mmoja wa wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi kwenda eneo la tukio kunaweza kuleta ushawishi kwa wajumbe wake hasa kwa yule aliyetoa kiasi kikubwa cha pesa. 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, ni lazima wakati wa zoezi la kwenda eneo lenye mgogoro kwa wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi Mkurugenzi wa Halmashauri husika aratibu zoezi hilo huku ratiba nzima ikiwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya katika kipindi cha mwezi mmoja. 

‘’ Jamaa anatoa laki mbili anayelalamika hana kitu unategemea hapo haki itatendekaje, ni marufuku kabisa na taratibu zote za kwenda uwandani zipitie kwa DC na ratiba ijulikane mapema’’ alisema Dkt Mabula. 

Akigeukia uzinduzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba katika wilaya ya Ulanga, Dkt Mabula alisema Serikali imezindua Baraza hilo ili kupeleka huduma karibu na kurahisisha usikilizaji kesi za ardhi kwa wananchi ambao baadhi ya maeneo wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kupata huduma hiyo na kubainisha kuwa sasa wananchi wa Ulanga watapata haki kwa wakati na kwa umbali mdogo. 

Aliwaasa wananchi wa wilaya ya Ulanga kulitumia vyema Baraza Ardhi na Nyumba lililozinduliwa na kuwataka kuhakikisha wanafuata taratibu zote za utatuzi wa migogoro ya ardhi pamoja na kuachana na ile migogoro ya kifamilia kwa kutumia Mabaraza ya Vijiji na Kata kushughulikia migogoro hiyo. 

Dkt Mabula aliusifu mkoa wa Morogoro kwa kutoa mafunzo kwa wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi na kubainisha kuwa mafunzo hayo yawe chachu kwa wajumbe wake kutenda haki wakati wa kufanya maamuzi kwa kuwa tayari wana weledi katika eneo hilo. 

Kwa upande wake Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini Stela Tulo alisema, uzinduzi wa Barazala la Ardhi katika wilaya ya Ulanga limejibu kiu ya muda mrefu ya wananchi wa wilaya hiyo kupata huduma kwa ukaribu ambapo awali iliwalazimu kusafiri umbali mrefu hadi Kilombero kupata huduma. 

Kwa mujibu wa Stela, kuzinduliwa kwa Baraza la Ulanga sasa kunaufanya mkoa mzima wa Morogoro kuwa na Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Manne (4) na kubainisha kuwa Baraza hilo sasa linaongeza idadi ya Mabaraza yanayofanya kazi nchini kufikia 54 kati ya 97 yaliyoidhinishwa. 

Msajili huyo wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini alisema, mkoa wa Morogoro pekee kwa sasa una Mashauri 2,500 ya ardhi kati ya 29,000 nchi nzima na kubainisha kuwa, kuzinduliwa kwa Baraza la Ulanga ni moja ya jitihada kuhakikisha Mashauri katika mkoa huo yanapungua kama siyo kuisha kabisa.

BENKI YA MAENDELEO TIB YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUINGIA MKATABA WA HUDUMA BORA KWA WATEJA WAKE

IMG_8635
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (katikati) akimkabishi mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Charles Singili (kulia) mara baada ya kuuzindua mkataba huo. Uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya Benki ya Maendeleo ya TIB.
IMG_8649
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto) akimkabidhi nakala ya mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter) Bw.Joseph Kidaha (katikati) mwakilishi wa wateja waliohudhuria uzinduzi rasmi wa Mkataba huo. 
IMG_8656
 Mkurugenzi, Mkakati na Mahusiano ya Kibiashara, Bw. Patrick Mongella (kulia) akipokea nakala za Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter) kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto).
IMG_8644
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Charles Singili (katikati) akionesha mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter) mara ya kukakidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto). Anayeshuhudia ni mmoja wa wateja wa benki hiyo, Bw.Joseph Kidaha (kulia).
IMG_8657
 IMG_8658
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya TIB wakifuatilia uzinduzi Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter).
IMG_8716
Baadhi ya wateja wa Benki ya Maendeleo ya TIB wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (katikati waliokaa) pamoja na menejimenti ya benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Charles Singili (wapili kulia waliokaa).

Na Mwandishi wetu
Benki ya Maendeleo TIB (TIB Development Bank) imeadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza kuadhimishwa tarehe 16 Juni, 2019 kwa kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customers’ Service Charter) ili kuendeleza kutoa huduma bora na zenye viwango kwa wateja wake.
Akizungumza wakati wa unzinduzi wa Mkataba huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Dkt. Mary Mashingo amesema kuwa malengo ya Mkataba huo ni kuendeleza kutoa huduma bora bila ya upendeleo, kwa heshima na kwa haraka.
“Huu ni Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Maendeleo TIB unaakisi dhamira ya dhati ya Benki ya kuwahudumia wateja bila ya upendeleo, kwa heshima na kwa haraka. Mkataba huu una ahadi za huduma mahsusi na za hiari.
Aliongeza kuwa Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Maendeleo TIB unatambua wateja wetu wana haki ya kuelewa kiwango cha huduma kinachotolewa na Benki yao kwa wakati wote.
Kwa mujibu wa Dkt. Mashingoo, Benki iko tayari kupokea maoni ya namna ya kurekebisha na kuboresha zaidi huduma zake.
“Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo TIB, tumejipanga kusimamia kwa dhati utekelezaji wa mkataba huu katika kutekeleza dhamira  ya Mheshimiwa  Rais ya  kuwa  na  taasisi za umma zinazowahudumia  wadau wake. Watumishi  wa  Benki mnatakiwa kufanya kazi  kwa weledi,  juhudi,  maarifa  na uadilifu  mkubwa.  Pamoja na utoaji wa huduma bora, kwa haraka na kwa staha ili kuwaondolea wananchi usumbufu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Charles Singili alisema kuwa TIB imejidhatiti katika kuimarisha mahusiano nawateja wake, hivyo kuzinduliwa kwa Mkataba huu kutachochea utendaji kazi wake ikizingatiwa kuwa benki hiyo muhimili muhimu katika kuunganisha Serikali na Sekta Binafsi.
“Zipo Benki za biashara lakini hii ya TIB ni tofauti kabisa kwa kuwa yenyewe imejikita katika kuleta maendeleo kwa wateja na watanzania kwa ujumla. Hivyo, mkataba huu utaimarisha mahusiano na wateja wetu,” amesema.
Ameongeza kuwa TIB ni benki kiunganishi muhimu kati ya Serikali na Sekta Binafsi, kwa kuchagiza uchangiaji kwa kiasi kikubwa katika masuala ya uwekezaji.
Akizungumzia kaulimbiu ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2019, isemayo “Uhusiano kati ya uwezeshaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji: Kujenga utamaduni wa Utawala Bora, matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika utoaji wa Huduma Jumuishi.” Bw. Singili ametoa wito kwa vijana kutumia uwepo wa taasisi wezeshi ili waweze kujikwamua katika kuinua vipato vyao na taifa kwa ujumla.
“TIB tumejikita katika kuwasidia vijana waweze kusimamia misingi ya utawala bora lakini pia kuangalia kwa namna ambavyo wanaweza kuzalisha mazao mbalimbali hali inayoweza kuwasaida kutimia malengo yao binafsi na ya serikali kwa ujumla hasa kupitia mkakati wa Tanzania ya viwanda,’’ alifafanua.
Kwa upande wa wateja wa benki hiyo waliowakilishwa na Bwa. Joseph Kidaha amesema kuwa, mkataba huo una maana kubwa kwa wateja wa benki hiyo huku akisisitiza kuwa,  ukisimamiwa vizuri utaleta manufaa makubwa kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.
“Ni jambo zuri kuona mahusiano mazuri yanatengenezwa kati ya benki na wateja wake, hiyo itaamsha ari kwa watu katika kuitafuta hudumu ya benki hii na tulio wengi kutimiza matarajio tuliyojiwekea ,’’ alisema.
Bwana Kidaha aliwataka wadau kuja kukopa katika benki ya TIB na kufanya marejesho kwa muda unaostahili ili kuwafanya watanzania wengi waendelee kunufaika na mikopo ya benki ya maendeleo (TIB)