Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo
(katikati) akimkabishi mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja Mkurugenzi
Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Charles Singili (kulia) mara baada ya
kuuzindua mkataba huo. Uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya
Benki ya Maendeleo ya TIB.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo
(kushoto) akimkabidhi nakala ya mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja
(Customer Service Charter) Bw.Joseph Kidaha (katikati) mwakilishi wa wateja waliohudhuria uzinduzi rasmi wa Mkataba huo.
Mkurugenzi,
Mkakati na Mahusiano ya Kibiashara, Bw. Patrick Mongella (kulia)
akipokea nakala za Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service
Charter) kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya
Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Charles Singili (katikati)
akionesha mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service
Charter) mara ya kukakidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa
Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto). Anayeshuhudia
ni mmoja wa wateja wa benki hiyo, Bw.Joseph Kidaha (kulia).
Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya TIB wakifuatilia uzinduzi
Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter).
Baadhi
ya wateja wa Benki ya Maendeleo ya TIB wakiwa katika picha ya pamoja na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt.
Mary Mashingo (katikati waliokaa) pamoja na menejimenti ya benki hiyo
wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Charles Singili (wapili kulia
waliokaa).
Na Mwandishi wetu
Benki
ya Maendeleo TIB (TIB Development Bank) imeadhimisha Wiki ya Utumishi
wa Umma iliyoanza kuadhimishwa tarehe 16 Juni, 2019 kwa kuzindua Mkataba
wa Huduma kwa Wateja (Customers’ Service Charter) ili kuendeleza kutoa
huduma bora na zenye viwango kwa wateja wake.
Akizungumza
wakati wa unzinduzi wa Mkataba huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa benki hiyo, Dkt. Mary Mashingo amesema kuwa malengo ya Mkataba huo ni
kuendeleza kutoa huduma bora bila ya upendeleo, kwa heshima na kwa
haraka.
“Huu
ni Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Maendeleo TIB unaakisi
dhamira ya dhati ya Benki ya kuwahudumia wateja bila ya upendeleo, kwa
heshima na kwa haraka. Mkataba huu una ahadi za huduma mahsusi na za
hiari.
Aliongeza
kuwa Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Maendeleo TIB unatambua
wateja wetu wana haki ya kuelewa kiwango cha huduma kinachotolewa na
Benki yao kwa wakati wote.
Kwa mujibu wa Dkt. Mashingoo, Benki iko tayari kupokea maoni ya namna ya kurekebisha na kuboresha zaidi huduma zake.
“Bodi
ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo TIB, tumejipanga kusimamia kwa
dhati utekelezaji wa mkataba huu katika kutekeleza
dhamira ya Mheshimiwa Rais ya kuwa na taasisi za umma
zinazowahudumia wadau wake. Watumishi wa Benki mnatakiwa
kufanya kazi kwa
weledi, juhudi, maarifa na uadilifu mkubwa. Pamoja na utoaji wa
huduma bora, kwa haraka na kwa staha ili kuwaondolea wananchi usumbufu.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw.
Charles Singili alisema kuwa TIB imejidhatiti katika kuimarisha
mahusiano nawateja wake, hivyo kuzinduliwa kwa Mkataba huu kutachochea
utendaji kazi wake ikizingatiwa kuwa benki hiyo muhimili muhimu katika
kuunganisha Serikali na Sekta Binafsi.
“Zipo
Benki za biashara lakini hii ya TIB ni tofauti kabisa kwa kuwa yenyewe
imejikita katika kuleta maendeleo kwa wateja na watanzania kwa ujumla.
Hivyo, mkataba huu utaimarisha mahusiano na wateja wetu,” amesema.
Ameongeza
kuwa TIB ni benki kiunganishi muhimu kati ya Serikali na Sekta Binafsi,
kwa kuchagiza uchangiaji kwa kiasi kikubwa katika masuala ya uwekezaji.
Akizungumzia
kaulimbiu ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2019, isemayo “Uhusiano
kati ya uwezeshaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji:
Kujenga utamaduni wa Utawala Bora, matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika
utoaji wa Huduma Jumuishi.” Bw. Singili ametoa wito kwa vijana kutumia
uwepo wa taasisi wezeshi ili waweze kujikwamua katika kuinua vipato vyao
na taifa kwa ujumla.
“TIB
tumejikita katika kuwasidia vijana waweze kusimamia misingi ya utawala
bora lakini pia kuangalia kwa namna ambavyo wanaweza kuzalisha mazao
mbalimbali hali inayoweza kuwasaida kutimia malengo yao binafsi na ya
serikali kwa ujumla hasa kupitia mkakati wa Tanzania ya viwanda,’’
alifafanua.
Kwa
upande wa wateja wa benki hiyo waliowakilishwa na Bwa. Joseph Kidaha
amesema kuwa, mkataba huo una maana kubwa kwa wateja wa benki hiyo huku
akisisitiza kuwa, ukisimamiwa vizuri utaleta manufaa makubwa kwa wateja
wake na watanzania kwa ujumla.
“Ni
jambo zuri kuona mahusiano mazuri yanatengenezwa kati ya benki na
wateja wake, hiyo itaamsha ari kwa watu katika kuitafuta hudumu ya benki
hii na tulio wengi kutimiza matarajio tuliyojiwekea ,’’ alisema.
Bwana
Kidaha aliwataka wadau kuja kukopa katika benki ya TIB na kufanya
marejesho kwa muda unaostahili ili kuwafanya watanzania wengi waendelee
kunufaika na mikopo ya benki ya maendeleo (TIB)
No comments:
Post a Comment