Mkemia
Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewasisitiza wakaguzi wa
kemikali na maabara za kemia kuzingatia ueledi, uadilifu na uaminifu
katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Mkemia
Mkuu wa Serikali amezungumza hayo leo wakati akifungua mkutano wa mwaka
wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia kutoka Mamalaka ya Maabara
ya Mkemia Mkuu wa Serikali unaofanyika Baraza la Maaskofu, Kurasini, Dar
es Salaam.
“Serikali
imetupa majukumu ya kusimamia Sheria ya Mamlaka ya Maaabara ya Mkemia
Mkuu wa Serikali, Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za
Viwandani na Majumbani na Sheria ya Vinasaba vya Binadamu, hivyo
tunapaswa kuzingatia ueledi, uadilifu, uaminfu na upendo ili kuhakikisha
tunatekeleza majukumu yetu kwa ufanisi.
Tutambue
Serikali yetu imejielekeza katika kujenga uchumi wa viwanda na
inajitahidi kuwekeza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara ikiwemo
wanaojihusisha na kemikali, hivyo tunapotekeleza majukumu yetu
tunapaswa kuelewa uelekeo huo wa Serikali na kufanya maamuzi kwa wakati
na haraka ili kutokwamisha wadau wetu huku tukizingatia Sheria.”
Aidha,
Mkemia Mkuu wa Serikali alisema Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti
inawapongeza wakaguzi hao kutokana na kazi kubwa wanayofanya na
inawahamasisha kuboresha zaidi huduma kwa wadau kwa kufuata Sheria,
taratibu na kanuni zinazowaongoza kama watumishi wa umma.
“Bodi
ya Wakurugenzi na Menejimenti inatambua mchango mkubwa wa wakaguzi
katika kusimamia Sheria na kuingiza maduhuli ambayo taasisi inatumia
katika kuboresha huduma na kujiendesha. Tunatambua changamoto zipo na
tunaendelea kuzifanyia kazi kama kuongeza watumishi na vitendea kazi.
Tuna maeneo ya msingi ya kuyawekea kipaumbele hasa kwenye uwekezaji wa
mitambo ya kisasa ya maabara na teknolojia ili kuwawezesha wakaguzi
kutoa huduma bora na za haraka kwa wadau. Tufanye kazi kama familia ili
kuweza kutekeleza majukumu yetu kwa mafanikio.” Alimaliza.
Akitoa
neno la shukrani, Mkaguzi wa Kemikali, Bw. Jovitus Mukela, alimshukuru
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko kwa nasaha nzuri za
ufunguzi wa Mkutano huo.
Kwa
niaba ya wakaguzi wenzangu tunakushukuru sana kwa nasaha na maneno
mazuri uliyotuambia maana pia yanatukumbusha majukumu yetu na napenda
kuwaomba wakaguzi wenzangu kuzingatia yale yote yaliyozungumzwa na
kushirikiana kutoa huduma nzuri, kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeitendea
haki Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, sisi wenyewe na nchi
kwa ujumla.” alimaliza
Mkemia
Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akiongea na
Wakaguzi wa kemikali (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa
Mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia ulioandaliwa na
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kufanyika leo katika
Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Kurasini, Dar es Salaam.
Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara za Huduma za Ubora wa
Bidhaa, Sabanitho Mtega, Maendeleo ya Biashara, George Kasinga,
Usimamizi wa Kemikali, Daniel Ndiyo na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi
Jinai na Huduma za Vinasaba, Elias Mulima.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Kemikali, Daniel Ndiyo (aliyesimama),
akizungumza na Wakaguzi wa Kemikali (hawapo pichani) kabla ya
kumkaribisha Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa tatu
kulia) kufungua Mkutano wa Mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali leo.
Wakaguzi
wa Kemikali na Maabara za Kemia wakimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali,
Dkt. Fidelice Mafumiko (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano
huo.
Mkaguzi
wa kemikali na Maabara za Kemia kutoka Maabara ya Kanda ya Kaskazini,
Jovitus Mukela (aliyesimama), akitoa neno la shukrani kwa niaba ya
wakaguzi mara baada ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufungua Mkutano huo.
Mkemia
Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyekaa katikati), akiwa
pamoja na Wakurugenzi na Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia kutoka
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali mara baada ya kufungua
Mkutano wa Mwaka wa Wakaguzi hao uliofanyika Ukumbi wa Baraza la
Maaskofu Katoliki Tanzania, Kurasini, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment