Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema ni vema Sekreatarieti ya Maadili ya
viongozi wa Umma iendelee kuwakumbusha viongozi na watumishi wa umma
nchini kutimiza wajibu wao ili kuweza kufikia malengo ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na
Serikali.
Mtaka ameyasema hayo Juni 03, 2019 Mjini Bariadi, wakati akifungua
mafunzo kwa Viongozi wa Umma mkoani Simiyu, ambayo yameandaliwa na
Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya
Magharibi Tabora.
Amesema ikiwa kila mmoja katika Utumishi wa Umma atatimiza wajibu wake
jamii na nchi kwa ujumla wake itaweza kufikia malengo yaliyowekwa na
Serikali katika nyanja mbalimbali kwa wakati.
“Ni vizuri Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiendelea
kuwakumbusha watu wote wanaofanya kazi zinazoihusu jamii kutimiza
wajibu wao, kila mmoja akitimiza wajibu wake yapo mambo mengi sana
sisi kama jamii, nchi, mkoa na kwa namna ambavyo uongozi na mgawanyiko
wa .nchi yetu ulivyo tutafikia malengo yetu kwa wakati” alisema Mtaka.
Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa Umma ambao ni watoa maamuzi katika
maeneo yao ya kazi kuwa makini katika kutoa maamuzi na wahakikishe
wanafanya maamuzi kwa wakati.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele
amesema viongozi wa Umma wanapaswa kutoa maamuzi kwa kuzingatia
sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa ili kutoiletea hasara
Serikali.
Ameongeza kuwa Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma itaendelea
kutoa elimu kwa viongozi wa umma juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi
ya uadilifu katika uongozi na endapo ikitokea kiongozi yeyote
atakengengeuka na kutofuata maadili sheria itachukua mkondo wake.
Kwa upande wake Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe.
Mary Mrio ameshukuru Sekretarieti ya Maadili kwa kutoa mafunzo ya
maadili kwa viongozi wa Umma na akatoa wito kwa viongozi hao kuwa
waadilifu, kutekeleza majukumu yao na kutojilimbikizia mali kinyume na
taratibu na maadili ya viongozi wa Umma.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe.
Bahame Kaliwa ametoa wito kwa Sekretarieti ya Maadili kwa viongozi wa
Umma kutoa elimu ya maadili kila viongozi wapya wanapoteuliwa au
kuchaguliwa, hususani madiwani wanapochaguliwa na kuunda Mabaraza
mapya ya madiwani ili wajue misingiya uadilifu inayopaswa kuwaongoza
katika kazi zao
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Umma
mkoani humo, wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora,
ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi
ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa
kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini
Bariadi.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na viongozi wa
Umma Mkoani humo, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora,
ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu
Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya
Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele, akizungumza na viongozi wa Umma
Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo
yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Afisa
Maadili kutoka Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya
Magharibi Tabora, Bw. Onesmo Msalangi akizungumza na viongozi wa Umma
Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo
yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi
ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa
kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini
Bariadi.
Hakimu
mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio akichangia
hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa
Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert
Lweyo akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya
Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi
Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03,
2019 Mjini Bariadi.
No comments:
Post a Comment