Na Stella Kalinga, Simiyu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imefungua rasmi Ofisi ya Kanda mpya
ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga
ambapo makao makuu ya kanda hiyo yatakuwa Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Kaimu
Meneja wa TFDA Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama amesema
mamlaka hiyo imeanzisha Kanda Mpya ya Ziwa Mashariki inayojumuisha
mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ili kusogeza huduma kwa wananchi na
kuharakisha ukuaji wa uchumi wa kati unaotegemea viwanda.
Amesema ofisi hii itajishughulisha na usajili wa maeneo yanayo
jihusisha na uzalishaji na uuzaji wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa
tiba, kupokea maombi ya usajili wa bidhaa za vyakula vinavyofungashwa,
kufanya ukaguzi wa bidhaa za vyakula katika soko kuwalinda walaji na
kudhibiti usindikaji wa chakula dawa na vipodozi.
Kazi nyingine zitakazofanywa na kanda hii ni kutoa vibali vya
uingizaji nchini na usafirishaji wa chakula nje ya nchi, kufanya
ufuatiliaji wa bidhaa za vyakula katika soko, kuhamasisha matumizi
sahihi ya dawa, vipodozi na vifaa tiba pamoja na kuelimisha na kutoa
taarifa kwa wadau na wananchi kwa ujumla kuhusu bidhaa zinazothibitiwa
na mamlaka.
Aidha, Mwasulama amesema Ofisi ya kanda hii itatekeleza majukumu yake
kwa kushirikiana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ambapo
wataalam waliopo kwenye wilaya, manispaa, miji na majiji watasimamia
sheria ya chakula na dawa kwa mujibu wa kanuni ya kukasimu baadhi ya
majukumu na madaraka ya TFDA katika Halmashauri.
Akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa wa Simiyu na TFDA katika
ufunguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni
vema Taasisi nyingine zinazohitajika katika uwekezaji wa viwanda na
maeneo mengine ya uwekezaji zikaiga mfano wa TFDA kwa kusogeza huduma
karibu na wananchi ili waweze kupata huduma kwa wakati.
“Hiki kilichofanywa na TFDA ni vizuri taasisi nyingine nazo ziige,
kama leo TFDA ipo Simiyu kama Kanda ya Ziwa Mashariki ningetamani
kuwaona TBS, NEMC, OSHA wako Simiyu kama Kanda ya Ziwa Mashariki na
Taasisi zote ambazo kwenye uwekezaji wa viwanda na maeneo mengine ya
uwekezaji zinakuwa karibu na maeneo ya kutolea huduma” alisisitiza
Mtaka.
Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa watumishi wa Mamlaka za
Serikali za Mitaa wanaotekeleza majukumu waliyokasimiwa na TFDA
kufanya majukumu hayo kwa mujibu sheria huku akiwaasa kuacha tabia ya
kufungia biashara za wananchi bila kuwaelimisha badala yake wawasaidie
kuwapa elimu ili wazalishe bidhaa bora kwa walaji.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Dkt. Mike Mabimbi
akizungumza kwa niaba ya waganga wakuu wa wilaya ambao ni Makatibu wa
kamati za ukaguzi wa chakula na dawa amesema watahakikisha wanasimamia
utekelezaji wa majukumu wanayokasimiwa na TFDA kwa mujibu wa sheria
na akashukuru TFDA kusogeza huduma karibu na wananchi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wataalam
wa Mkoa huo Mamlaka ya Chakula na Dawa, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya
Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu,
Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi
umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu
Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi.
Nuru Mwasulama akitoa taarifa fupi ya uanzishwaji wa Kanda hiyo
itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake
yakiwa Bariadi Mjini, katika uzinduzi waa kanda hiyo uliofanyika Juni
20, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi
ya wataalam wa mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA)
wakifuatilia masuala mbalimbali ambayo yaliyokuwa yanaendelea katika
Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia
mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi
Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi
ya viongozi, wataalam wa mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Chakula na
Dawa(TFDA) wakifuatilia masuala mbalimbali ambayo yaliyokuwa yanaendelea
katika Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki
itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake
yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimueleza jambo Kaimu Meneja wa
Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru
Mwasulama mara baada ya kuzindua rasmi Kanda ya Ziwa Mashariki ya
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara
na Shinyanga, Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu
Mganga mkuu wa Mkoa, Dkt. Mugune Maeka akitoa neno la shukrani mra
baada ya kuhitishwa kwa uzinduzi wa Kanda ya Ziwa Mashariki ya Mamlaka
ya Chakula na Dawa(TFDA) itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na
Shinyanga, Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati mbele) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi, wataalam wa mkoa wa Simiyu na
Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) mara baada ya Uzinduzi wa Ofisi ya
Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu,
Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi
umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na
baadhi ya wataalam wa Mkoa huo Mamlaka ya Chakula na Dawa, wakati wa
uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki
itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake
yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
No comments:
Post a Comment