Zanzibar imepiga hatua katika kudhibiti maambukizo ya virusi
vinavyosababisha kutokana na takwimu zinazoonesha mambukizi ya virusi
hivyo kuwa chini ya asilimia moja (1%) ambapo kwa upande wa unguja ni
0.5% wakati kisiwa cha pemba kufikia 0.2%.
Mkurugenzi Mtendaji wa tume ya Ukimwi Zanzibar Dk. Ahmed Momahed
Khatib alieleza hayo katika ziara ya kushtukiza iliofanywa na katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif
Mohamed kupitia Idara mbali mbali zilizo chini ya Ofisi hiyo.
Dk. Ahmed alisema Takwimu hizo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa
mwaka 2016/2017 ambapo kwa sasa tume hiyo bado inaendelea na jukumu la
kutoa elimu kwa wananchi dhidi ya hatua za kuchukua katika kujikinga
na virusi vinavyosababisha maradhi hayo.
Alifafanua kuwa kwa sasa bajeti ya tume hiyo imefanikiwa kutegemea
bajeti ya ndani kwa asilimia kubwa kutokana na serikali ya Mapinduzi
Zanzibar kuongeza nguvu katika bajeti ya tume hiyo kila mwaka mpya wa
fedha hali iliyopelekea kupunguza kutegemea Mataifa na Taasisi
wahisani.
Nae Afisa kitengo cha sera , mipango na mwiitiko wa kijamii wa tume
hiyo Bibi Jogha Bakari Mohamed alisema uwepo wa changamoto ya wananchi
wengi nchini hususani vijana kwa kulichukulia tatizo la maambukizi ya
ukimwi kama jambo la kawaida na kufanya mambo yao bila ya kujali
kuchukua tahadhari yoyote jambo linalopelekea kuenea kwa maambukizi.
Mkuu huyo wa kitengo alisema ni jambo linalosikitisha kuona kesi mpya
nyingi zinawahusu vijana wengi wanaoripotiwa kuwepo katika hali
hatarishi inayosikitisha na kuhuzunisha ikizingatiwa kuwa wao ndio
nguvu kazi na tegemeo la Taifa katika masuala ya Maendeleo ya nchi.
Katika ziara hiyo ya kushtukiza watendaji wa tume ya ukimwi walipata
fursa ya kuelezea faraja yao pamoja na changamoto zinazowakabili kwa
Katibu Mkuu ikiwemo changamoto ya kuchelewa kukamilika kwa mfumo
maalum wa kutunzia kumbukumbu zao. {Data Base System}.
Wakati huo huo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
alizitembelea ofisi za idara ya watu wenye ulemavu na kumtaka
mkurugenzi wa idara hiyo kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa mujibu wa
mahitaji yao ambao wanatarajiwa kupangwa katika ofisi za wilaya.
Nd. Mkuu Shaaban amewaeleza watendaji wa Taasisi hiyo kufanya kazi kwa
uwadilifu kwa kuzitunza vyema nyaraka za ofisi zao sambamba na
kuziwasilisha barua zinazoingia idarani mwao kwa wakati badala ya
kusubiri mrindikano wa barua hizo, kwani kufanya hivyo kutasaidia
mambo muhimu na ya msingi kuchukuliwa hatua bila ya kuchelewa.
Pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu Shaaban amelezea kukerwa kwakwe na
mpangilio mbaya ya utunzaji wa baadhi ya kumbukumbu na nyaraka katika
idara ya watu wenye ulemavu na kuagiza hatua za haraka kuchukuliwa ili
kuzinusuru nyaraka hizo kupotea.
Mapema Katibu Mkuu akibadilishana mawazo na watendaji wa tume ya
uchaguzi Zanzibar wakimueleza kuwa kwa sasa tume ipo katika mchakato
wa kuimarisha kitengo chake cha mfumo wa teknolojia kwa ajili ya
kukamilisha zoezi la usajili linalotarajia kuanza hivi karibuni.
Watendaji hao walimueleza katibu mkuu uwepo wa changamoto kwa wapiga
kura wengi kutokana na kutokuwa na elimu ya upigaji kura ingawaje tume
ya uchaguzi inaendelea na utowaji wa elimu hiyo hali inayosababishwa
na ukubwa wa Maeneo ya Zanzibar ikilinganishwa na idadi ya watendaji
wa tume hiyo.
Ziara hiyo ya kushtukiza ya Katibu Mkuu imejumuisha tume ya ukimwi
Zanzibar, Idara ya watu wenye ulemavu pamoja na tume ya uchaguzi ziara
ambayo ina lenga kuimarisha utendaji kazi wa idara zilizo chini ya
ofisi ya makamu wa Pili wa Rais.
Katibu
Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd.
Shaaban Seif Mohamed akizungumza na Wafanyakazi wa Idara ya Watu wenye
ulemavu katika ziara ya kushtukizia.
Mkurugenzi
wa Idara ya Watu wenye ulemavu Abeda Rashid Abdulla akimuelezea Nd.
Shaaban majukumu ya Idara hiyo lipofanya ziara ya kushtukizia.
Mkuu
wa Utawala wa Tume ya Uchaguzi Nd. Saadon Ahmed Khamis akizungumza na
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban
Seif.
Katibu
Mkuu Shaaban akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi
Zanzibar Nd. Thabit Idarous Faina alipotembelea Ofisi hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa tume ya Ukimwi Zanzibar Dk. Ahmed Momahed Khatib akimueleze
Katibu Mkuu Shaaban hali halisi ya Ukimwi ilivyo Zanzibar.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Tume ya Ukimwi Zanzibar wakimsikiliza Katibu Mkuu wakatialipofanya ziara ya Ghafla kwenye Ofisi yao.
Mtendaji
wa Tume ya Ukimwi Zanzibar akimuelezea Ndugu Shaaban changamoto
wanazopambana nazo katika kuwapatia elimu Wananchi hasa Vijana.
Nd.
Shaaban akisisitiza umuhimu wa kutunzwa kumbukumbu alipozungumza na
Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofiosi yake. Picha na – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment