Waziri
wa Viwanda na Uwekezaji Sudan Kusini Ndugu Paul Mayomu atembelea Mradi
wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa-SGR kipande cha Daresalaam - Morogoro,
Ziara hiyo imefanyika hivi karibuniJune , 2019.
Aidha,
katika ziara hiyo iliongozwa na mwenyeji wake Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe, walipata fursa ya kuona
maendeleo na hatua tofauti za ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR ukiwemo
ujenzi wa stesheni kuu ya Daresalaam, madaraja, na utandikaji wa reli
unao endelea maeneo ya vingunguti jijini Dar Es Salaam.
Waziri
Mayomu ameipongeza Tanzania kwa kuamua kujenga Reli ya Kisasa - SGR
ambayo ni muhimu katika kuchochea maendeleo ya uchumi, viwanda na
biashara katika Taifa na nchi jirani.
Hata
hivyo, Waziri Mayomu ameeleza kuwa reli hii itakapo kamilika itakuwa
chachu ya maendeleo kwa nchi zote mbili pia itadumisha uhusiano katika
sekta ya uchukuzi, viwanda na biashara kati ya Tanzania na Sudan ya
Kusini.
Kwa
upande wake, Waziri Kamwelwe amempongeza waziri Mayomu kwa kuja
Tanzania ambayo ni heshima kwa Taifa na kujionea maendeleo yanayofanyika
katika sekta ya usafirishaji na uchukuzi katika ujenzi wa reli ya
kisasa ambayo ni chachu ya maendeleo baina ya nchi hizo mbili.
Waziri Kamwelwe ameahidi kudumisha uhusiano kupitia reli ya kisasa hasa katika sekta ya viwanda, biashara na uchumi.
No comments:
Post a Comment