Waziri
wa Katiba na Sheria Dkt Balozi Augustine Mahiga amepokea ripoti ya
mapendekezo ya sheria yaliyowasilishwa na Tume ya Kurekebisha Sheria hii
leo Jijini Dodoma.
Akipokea
taarifa hiyo Dkt Balozi Mahiga amefurahishwa kwa kazi nzuri iliyofanywa
na Tume hiyo pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha kukamilika kwa
mapendekezo ya sheria ya Ufilisi na nyingine zilizowasilishwa katika
tume hiyo ambazo ni sheria ya Ushahidi na ile ya Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro.
‘’Nimeridhishwa
kwa kazi nzuri iliyofanyika kwani tunakwenda kupata sheria madhubuti
itakayoendana na hali ya sasa na kusimamia kikamilifu misingi ya utawala
bora’’. Alisema Balozi Mahiga.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Mhe, Januari
Msofe amesema kuwa tume yake imefanya mapitio na utafiti wa kina kuhusu
mifumo ya Sheria zinazosimamia Ufilisi na kubaini mapungufu ya kisheria
na kiutendaji ambao umeathili utekelezaji wa masuala ya hayo hapa
Nchini.
Ameendelea
kubainisha mapungufu hayo ni pamoja na kuwepo kwa sheria mbalimbali za
kisekta kama vile sheria ya Makampuni sura ya 212, sheria ya mabenki na
taasisi za kifedha sura ya 342 , sheria ya vyama vya ushirika sura ya
211, Sheria ya bima sura ya 394, sheria ya mashirika ya umma Sura ya 57
na sheria ya usajili wa wadhamini sura ya 318 na hivyo kukosekana kwa
sheria mahsusi inayosimamia jukumu la ufilisi pekee na kusababisha
mkanganyiko kwa watumiaji kufanya maamuzi ya sheria ipi inaweza kutatua
matatizo yanayowakabili.
Hata
hivyo kuwepo kwa sheria hizo kumesababisha matatizo kwa wadai kutojua
taratibu za kupata haki zao kwa wakati pamoja na kuwepo kwa taratibu
ndefu zinazochelewesha mashauri ya ufilisi kumalizika kwa wakati mara
baada ya taasisi au kampuni husika kufilisika.
Ameongeza
kuwa Sheria zinazotumika hivi sasa zimepitwa na wakati ambazo baadhi
yake zinatoa adhabu na faini ndogo kwa wale wanaokiuka taratibu za
ufilisi kwa mfano faini ya shilingi 200 kiasi ambacho hakiendani na
kiwango cha uchumi na maisha ya sasa huku zikitambua njia moja tu ya
mawasiliano ambayo ni posta pekee huku ikiacha nyuma maendeleo makubwa
upande wa teknolojia ya habari na mawasiliano.
Vilevile
Ugumu wa taratibu za kisheria katika ufilisi wa makampuni ya nje yenye
kampuni tanzu Tanzania na hivyo kuziachia kampuni hizo kutumia sheria za
nchi zao na kusababisha tatizo la kiuchumi katika nchi yetu kutokana na
sheria zetu kukosa nguvu ya kuyadhibiti makampuni hayo tofauti na nchi
jirani ya Kenya na Uganda ambazo zimeweka sheria na taratibu nzuri za
kufuata kwa makampuni ya nje yenye kampuni tanzu kwenye nchi zao.
Mapungufu
ya sheria hizo pia kumesababisha Kuwepo kwa mamlaka na vyombo
mbalimbali vinavyosimamia masuala ya ufilisi kama vile kuangalia mali za
kampuni pale inapofikia hatua ya kufilisika na mahakama kuteua chombo
au taasisi yoyote inayoshughulika na ufilisi badala ya Taasisi ya RITA
ambayo kisheria ndiyo yenye mamlaka kisheria ya kuwa msimamizi na
mratibu wa masuala yote ya ufilisi.
Hafla
ya kukabidhi ripoti hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya Wakuu wa Taasisi,
Watumishi wa Wizara ya katiba na sheria, Wakala wa Usajili Ufilisi na
Udhamini, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pamoja Wizara ya Ardhi.
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt, Balozi Augustine Mahiga akimkabidhi
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya RITA Prof. Hamisi Dihenga ripoti ya
Mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya Ufilisi mara baada ya
kukabidhiwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria hii leo
Jijini Dodoma, wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof.
Sifuni Mchome (wa tatu kutoka kulia) na Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu wa
RITA Emmy Hudson (wapili kutoka kulia).
Waziri
wa Katiba na Sheria Dkt, Balozi Augustine Mahige akikabidhiwa ripoti
kuhusu Mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya Ufilisi kutoka kwa
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Januari Msofe hii leo Jijini
Dodoma.
Kikao cha uzinduzi wa bodi kikiwa kinaendelea
No comments:
Post a Comment