Matokeo chanyA+ online




Friday, June 21, 2019

ZIWA NATRON KUPANDISHWA HADHI KUWA PORI LA AKIBA



 Wajumbe wa Bodi ya TAWA wakiangalia baadhi ya viumbe na Samaki aina ya Alcolapia wanaopatikana Ziwa Natron RAMSAR SITE lilipo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba.
Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dk. James Wakibara akijambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Meja Jeneral Mstaafu Hamis Semfuko, Bodi hiyo ilitembelea eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba.
 Mkuu wa wilaya ya Longido mkoani Arusha Frank Mwaisumbe mwenye (Kaunda suti) akiwa na Wajumbe wa Bodi ya TAWA wakiongozwa na Mwenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko kulia. Bodi hiyo ilitembelea eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba.

 Muikolojia wa eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE John Sule akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko kushoto, wajumbe wa bodi hiyo wametembelea eneo hilo linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori Tengefu ili kuliongezea thamani ya kiutalii. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko akiruka maji kwenye eneo chepechep la Ziwa Natron RAMSAR SITE lilipo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha, linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori Tengefu.
Na Ripota Wetu, ARUSHA

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imejipanga kulipandisha hadhi eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE kutoka aneo la ardhi owevu na kuwa eneo maalumu la Uhifadhi.

Hatua hiyo imelenga kunusuru hatari ya kutoweka kwa ndege maarufu duniani aina ya flamingo kutokana na shughuli mbalimbali za kibinaadamu zinazoendelea kufanywa pembezoni mwa Ziwa hilo.

Bodi ya TAWA ikiongozwa na Mwenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko imetembelea eneo hilo na kujionea hali halisi ya mazingira na maisha ya viumbe hai wanaopatikana eneo hilo maarufu duniani.

Eneo hilo ni maarufu duniani kwa kuwa na makazi Heroe wadogo kwa asilimia 100 wanaopatikana Afrika Mashariki na mazalia ya asilimia 80 ya Heroe wadogo wanaopatikana eneo hilo pamoja na aina tatu ya za Samaki aina ya Alcolapia.

Aidha eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE pia limekuwa muhimu kwa utalii wa ndege aina ya Heroe Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment