Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akitoa hotuba yake wakati wa
hafla ya utiaji saini wa DAWASA na wakandarasi juu ya ujenzi na
uendeshaji wa miradi sita mikubwa ya usambazaji wa maji yenye thamani ya
Bilion 114.5 iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert
Kajuna - Kajunason/Michuzi TV.
Wageni waalikwa na wafanyakazi wa DAWASA wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Prof Mbarawa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA)
Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwasilisha taarifa fupi ya miradi sita
mikubwa yenye thamani ya Bilion 114.5 kwa Waziri wa Maji Prof Makame
Mbarawa wakati wa halfa iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Miradi hiyo
itahudumia maeneo ambayo hayana kabisa mtandao wa DAWASA pamoja na Mkoa
wa Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA)
Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akibadilishana mkataba wa utekelezaji
wa miradi ya majisafi toka kwa wawakilishi wa makampuni ya ukandarasi ya
Watanzania na Wachina yatakayotekeleza ujenzi wa miradi itakayojengwa
Dar es Salaam na Pwani. Wengine wanaoshuhudia ni Mawaziri, Naibu Waziri,
Mwakilishi wa benki ya Dunia na viongozi wa serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/Michuzi
TV.
Wageni waalikwa na wafanyakazi wa DAWASA waliohudhuria hafla hiyo. Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jaffo akitoa machache. Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akifafanua jambo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akielezea furaha yake
juu ya DAWASA kupeleka wa maji katika jimbo lake la Mkuranga na
vitongoji vyake kupitia miradi hiyo. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenarali Mstaafu Davis Mwamunyange akielezea chagamoto zinazoikabili mamlaka hiyo.
Wageni waalikwa na wafanyakazi wa DAWASA waliohudhuria hafla hiyo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Assumpta Mshama ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha akitoa salamu.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sophia Mjema ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ilala akitoa salamu.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba akielezea furaha yake jinsi
DAWASA inavyotekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi kumtua mama ndoo
kichwani.
Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Selemani Jaffo (kushoto) akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja
(kulia).
Na Zainab Nyamka na Cathbert Kajuna, Michuzi TV.
Mamlaka
ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wametia saini mikataba
wa miradi mikubwa sita ya usambazaji maji kwa mkoa wa Dar es Salaam na
Pwani wenye thamani ya Bilion 114.5. Utiaji huo wa saini umefanyika leo
Julai 2, 2019 katika ofisi za Mamlaka hiyo huku ukishuhudiwa na Waziri
wa Maji Prof Makame Mbarawa, Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Waziri wa
TAMISEMI Selemani Jaffo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah
Ulega, Bodi ya DAWASA ikiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis
Mwamunyange na Wakuu wa Wilaya kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Kabla
ya utiaji saini, Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa amewataka Mamlaka
hiyo kusimamia vizuri miradi yote na kutafuta wakandarasi watakaofanya
kazi kwa uweledi na kumaliza kwa wakati na muda mfupi ili wananchi
wapate majisafi na salama. "Mamlaka mnaposimamia vizuri miradi ya maji,
na kupata mkandarasi atakayefanya kazi kwa weledi na kumaliza ujenzi wa
mradi kwa muda mfupi basi wananchi watapata majisafi na salama," amesema
Prof. Mbarawa.
Profesa
Mbarawa amesema, li kufikia lengo la serikali la kumtua mama ndoo
kichwani kwa asilimia 95 kwa mijini na asilimia 85 kwa vijijini na hilo
linawezekana iwapo miradi midogo na mikubwa kusimamiwa vizuri na
wakandarasi kumaliza kazi kwa wakati. Akitoa taarifa fupi ya miradi
hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema
kwa sasa mkoa wa Dar es Salaam unapata maji kwa asilimia 85 na
kukamilika kwa miradi hiyo mikubwa itafikia malengo ya serikali ya
asilimia 95 kufikia mwaka 2020.
Amesema,
katika kutekeleza miradi hiyo fedha zinazotumika ni za ndani
zinazotokana na makusanyo ya mapato ya kila mwezi ambapo ndani ya miaka
nne wameweza kuongeza ukusanyaji kutoka bilioni 3.2 hadi 11.2 kwa mwezi
na asilimia 35 za mapato zinatumika kwenye ujenzi wa miradi ya maji. Nae
Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenarali Mstaafu Davis Mwamunyange
ameeleza changamoto mbalimbali ndani ya mamlaka hiyo ila ameahidi
kushirikiana na menejimenti kukabiliana nazo ikiwemo upotevu wa maji na
wateja kupewa ankara za maji tofauti na matumizi yao.
Miradi
iliyowekewa saini ni mradi wa bomba la kusafirisha maji kutoka Jeti
hadi Buza wenye wenye urefu wa Km 7.5 na litahudumia maeneo ya Kiwalani
Vituka, Buza, Mashine namba 5 - Tandika na Mwanagati na wakazi 173,810
wa kata za Vituka na Buza watapata huduma ya maji kwenye awamu ya
kwanza.
Mradi
mwingine ni mradi wa usambazaji maji utakaoanzia matanki ya Chuo Kikuu
mpaka Bagamoyo awamu ya pili, mradi wa kuchimba visima 20 vya Kimbiji
Mpera, mradi wa usambazaji maji Kisarawe hadi Pugu, mradi wa maji katika
mji wa Mkuranga na mradi wa bomba la kusafirisha maji kutoka Mlandizi
(Ruvu juu) hadi Kijiji cha Mboga Chalinze. Viongozi mbalimbali hususani
wawakilishi wa wananchi wameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya
Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwezesha miradi mikubwa kama hiyo kwenda
katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na kutekeleza ilani ya Chama cha
Mapinduzi (CCM).
No comments:
Post a Comment