TANTRADE wapongezwa kwa kuyatendea haki maonesho hayo kila mwaka
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
Maonesho
ya 43 ya biashara maarufu kama sabasaba yenye kauli mbiu ya usindikaji
wa mazao ya kilimo kwa maendeleo ya viwanda yamezinduliwa rasmi leo
jijini Dar es Salaam huku masuala ya utafutaji wa masoko pamoja na
kuelimimisha wafanyabiashara kuhusiana na kliniki ya biashara yakitiliwa
mkazo.
Akizungumza
katika ufunguzi huo makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa
maonesho hayo ni kwa kutoa kipaumbele kwa bidhaa zinazozalishwa nchini
Kama Rais anavyosisitiza.
Suluhu
amesema kuwa maonesho ya sabasaba ni makubwa katika ukanda wa Afrika na
katika maonesho hayo zaidi ya nchi 35 zimeshiriki katika hali
inayoashiria ubora na utulivu unaovutia uwekezaji katika nchi yetu.
Amesema
kuwa serikali itaviwezesha viwanda vidogo na Kati katika masoko pamoja
na kuendelea kushiriki katika maonesho hayo ili waweze kutangaza bidhaa
zao zaidi.
Pia
amesema kuwa kukua kwa uchumi kwa asilimia 7 kunachagizwa na maendeleo
ya viwanda na kasi zaidi pamoja na wasimamizi wa sekta hiyo utapelekea
wananchi kufanana na kasi ya ukuaji wa uchumi.
Aidha
amezitaka mamlaka za TFDA, TBS, mamlaka za uvuvi na kilimo kufanya kazi
kwa uadilifu na utii na wao kama Serikali watasimamia na kuhakikisha
hakuna urasimu katika hilo, na amewahimiza tantrade ambao ndio
wasimamizi na waandaaji wa maonesho hayo kutafuta masoko na kutoa elimu
kwa wananchi kuhusiana na ubora na kuhamasisha matumizi ya bidhaa
zinazozalishwa nchini.
Kuhusiana
na ujenzi wa viwanda Suluhu amesema kuwa azma ya serikali katika ujenzi
wa viwanda bado ipo palepale na hiyo ni pamoja na utafutaji wa masoko
ya ndani na nje.
Kwa
upande wake Katibu mkuu wa chama Cha mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally
amewapongeza bodi, baraza na wafanyakazi wa tantrade kwa kuyatendea haki
maonesho hayo mwaka hadi mwaka.
Amesema kuwa maonesho ya namna hayo ni kisiwa Cha kuboresha nyaraka za kisera zinazosaidia katika maendeleo.
Pia
Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amesema kuwa gurudumu
la maendeleo linaenda vyema na hiyo ni kutokana na uongozi Bora wa
serikali ya awamu ya tano na kusema kuwa wizara za biashara na viwanda
pamoja na uvuvi na kilimo zinategemewa na watanzania wengi hivyo
zitazidi kusimamiwa ili kuongea kipato zaidi.
Bashungwa
amehaidi ushirikiano baina yao na wawekezaji na ndani na nje ya nchi na
kuwahimiza watanzania kushiriki katika ujenzi wa taifa kwa kujihusisha
na viwanda hasa vidogo na vya Kati.
Aidha
amezitaka halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji
na wao Kama wizara watahakikisha uwepo wamaeneo ya usindikaji.
Ufunguzi
huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, wakuu wa
Wilaya, wabunge pamoja na wajumbe wa baraza la wawakilishi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza wakati wa uzindua rasmi wa maonesho ya 43 ya Kimataifa ya
Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es
salaam leo Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizindua rasmi kwa kubonyeza kitufe maonesho ya 43 ya Kimataifa ya
Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es
salaam Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akitoa zawadi kwa washindi wakati wa uzinduzi rasmi na kutembelea
maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba
Barabara ya kilwarod jijini Dar es salaam Julai 02, 2019. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akitembelea mabanda mablimbali mara baada ya kuzindua rasmi maonesho ya
43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya
kilwarod jijini Dar es salaam Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment