Mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti
wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela wamejipanga kuwadhibiti
majangili wote na akiwa ameshika silaha bora ambazo wanazitumia walinzi wa hifadhi Village Game Scouts
ambao wanafadhiliwa na shirika la STEPS
Mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti
wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela akiwa pamoja na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Hashimu Komba wakiwa kwenye picha moja na viongozi na walinzi wa hifadhi Village Game Scouts
Mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti
wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela wamejipanga kuwadhibiti
majangili wote ambao wamekuwa wakifanya uharifu kwenye maliasili na misitu
iliyopo katika wilaya hiyo.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti
wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela wamejipanga kuwadhibiti
majangili wote ambao wamekuwa wakifanya uharifu kwenye maliasili na misitu
iliyopo katika wilaya hiyo.
Akizungumza wakati alipofanya ziara
ya ghafla ya kuwatembelea na kuwapa moyo walinzi wa hifadhi Village Game Scouts
ambao wanafadhiliwa na shirika la STEPS kwa kazi kubwa wanayofanya ya kulinda
maliasili zilizopo katika wilaya hiyo.
“Mimi niwapongeze sana maana
mnafanyakazi kubwa sana kupambana na majangili huko porini jambo ambalo
mnapaswa kupongezwa kwa namna yoyote ile” alisema Kasesela
Kasesela alisema kuwa hifadhi hizo zimekuwa
zikivamiwa na majangili hasa pembezoni mwa hifadhi hizo kutokana na kuwa jirani
na wakazi ambao wamekuwa wakifanya uharifu huo kutokana na tamaa zao.
Kasesela aliwaonya majangili kwamba
sasa wasirogwe kuingia kwenye mbuga za wanyama kutaka kufanya ujangili wa aina
yoyote kwakuwa wanamifumo ya kisasa zikiwemo kamera zimefungwa kwenye maeneo ya
mbuga hizo.
“Yoyote atakaye kamatwa kwa ujangili
atafikishwa kwenye vyombo husika na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa
atakuwa amefanya uharifu ambao haukubariki kisheria” alisema Kasesela
Aidha Kasesela alilipongeza shirika la STEPS kwa kuwafadhili walinzi wa hifadhi Village
Game Scouts kwa kuwapa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kazi hiyo ya ulinzi kwenye
mbuga zilizopo katika wilaya ya Iringa.
No comments:
Post a Comment