Mkuu
wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro ametembelea na
kukagua nyumba 10 za kisasa za makazi ya askari polisi zilizojengwa
katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga na kugharimu
shilingi milioni 225.
Mkuu
huyo wa jeshi la polisi amekagua nyumba hizo leo Jumanne,Julai 10,2019
na kueleza kuridhishwa jinsi zilivyojengwa kwa umaridadi na ubora wa
hali ya juu.
Nyumba
hizo 10 ni sehemu ya nyumba 114 ambazo ujenzi wake umekamilika nchi
nzima ikiwa ni sehemu ya nyumba 400 zinazojengwa maeneo mbalimbali
nchini kwa ajili ya makazi ya askari polisi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro akizungumza wakati
akikagua nyumba 10 za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo
la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga leo Jumanne Julai
10,2019.Kulia ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard
Abwao,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack.
"Ujenzi
huu umegharimu shilingi milioni 225,ni kweli nyumba hizi ni nzuri
sana,nimpongeze sana Mhe. Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe.Zainab Telack na
kamati yake ya ulinzi na usalama,kamati ya ujenzi na wadau wote
walioshiriki kwa kazi hii nzuri"
Muonekano wa nyumba za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
"Sasa
tunamsubiri Mhe. Rais,Dkt.John Pombe Magufuli muda siyo mrefu atazindua
hizi nyumba 114 nchi nzima. Pesa zilizotolewa ni kwa ajili ya kujenga
nyumba 400,lakini mpaka sasa zilizokamilika sasa ni 114",alisema IGP
Sirro.
Kwa
upande wake,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack alimshukuru
Rais Magufuli kwa kutoa pesa kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya askari
polisi huku akimuomba IGP Sirro kutafuta pesa kwa ajili ya ukarabati wa
baadhi ya nyumba za askari ambazo hali yake siyo nzuri.
Nyumba za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Muonekano wa nyumba za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga.
Kushoto
ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akimuonesha Mkuu wa
Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro nyumba za makazi ya
askari polisi zilizojengwa katika eneo la kambi ya polisi Kambarage
Mjini Shinyanga.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro akikagua nyumba za
makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la kambi ya polisi
Kambarage Mjini Shinyanga.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro akikagua nyumba za
makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la kambi ya polisi
Kambarage Mjini Shinyanga.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro akisamiliana na
waendesha bodaboda katika eneo la nyumba za makazi ya polisi Kambarage
Mjini Shinyanga na kuwakumbusha kuzingatia sheria za usalama barabarani
na kuwasihi kuacha kubeba mishikaki,wavae kofia ngumu na wawe na leseni.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment