Matokeo chanyA+ online




Wednesday, July 24, 2019

MLOGANZILA WAPATIWA MAFUNZO DHIDI YA MAJANGA YA MOTO

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Peter Mwambene (kushoto) akiwapatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto watumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, kulia ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Elinimo Shang’a.
Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wamepatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwa lengo la kujikinga na majanga ya moto na kuhakikisha Tanzania inakua salama dhidi ya majanga ya moto.

Watumishi wa Hospitali ya Mloganzila wakifuatilia mafunzo hayo 
Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo ni yanadharia na vitendo yametolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Elinimo Shang’a akielezea majanga ya moto yanavyotokea na namna ya kukabili.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Peter Mwambene amesema moja ya vitu vinavyomfanya mtu ashindwe kupambana na moto ni uoga na kutokua na vifaa sahihi vya kupambana na moto unapokua katika hatua za awali. 

Kamanda Shang’a akifundisha kwa vitendo namna ya kuzima moto kwa kutumia blanket maalum ya kuzimia moto (fire blanket).
Hivyo mafunzo hayo yatawajengea uelewa wa matumizi sahihi ya vifaa vya kuzimia moto, kujua aina mbalimbali za moto na namna ya kukabili, kujua mbinu za kuzima moto pamoja na namna ya kujiokoa pindi moto unapotokea.

Kamanda Shang’a akielekeza namna ya kuzima moto kwa kutumia kizimia moto aina ya poda kavu (dry powder fire extinguisher).
“Moto unapotokea mtu hushindwa kuukabili kutokana na uoga, unatakiwa ufanye yafuatayo pindi unapogundua moto, piga king’ora, kengele au mayowe,ita Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia namba 114, watu wasiojiweza wapewe kipaumbele kutoka eneo hatarishi, jaribu kuzima moto bila kuhatarisha usalama wako na watu wengine’’ amesema Mwambene.

Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mloganzila wakifanya zoezi la kuzima moto mara baada ya kupatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto.
Ametaja vyanzo vikuu vinavyoweza kusababisha majanga ya moto kuwa ni matumizi ya vifaa vya umeme visivyokua na ubora, ajali, nguvu asilia (radi, upepo,mkali, tetemeko la ardhi , milipuko ya Volkano).

Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mloganzila wakifanya zoezi la kuzima moto mara baada ya kupatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto.

Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mloganzila wakifanya zoezi la kuzima moto mara baada ya kupatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto.







No comments:

Post a Comment