Zaidi
ya shilingi bilion 2.8 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa
shule ya secondary ya elimu maalumu katika eneo la chuo cha Patandi
kilichopo Tengeru wilaya ya Arumeru mkoani Arusha
Akizungumza
wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya miundombinu wilayani
Arumeru Mkuu wa wilaya hiyo Mh, Jery Muro amesema kuwa fursa hiyo ni ya
kwanza hapa nchini ambapo italeta manufaa kwa watu wenye mahitaji
maalumu
Amesema
kuwa licha ya kusaidia kitaleta kielelezo cha kuhakikisha watoto wenye
ulemavu watapewa mtazamo mpya wa elimu kwa kuokoa watoto wenye
changamoto na mahitaji maalumu kutoka sehemu mbalimbali
Aidha
ameseama kila mwezi serikali inatoa bilioni 23 kwa wastani kwa ajili ya
ujenzi wa elimu na kugharamia sera ya elimu bure hapa nchini
Kwa
upande wake Mkuu wa shule ya mahitaji maalumu Patandi Mwl. Janeth Molel
ameipongeza serikali kwa juhudi kubwa za kuwajali watu wenye mahitaji
maalumu hasa kupitia elimu kwani hii itasaidia kupunguza ongezeko la
watoto wa mtaani na hatiamye kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda
Amsesema
kuwa,kwa sasa yamekamilika madarasa manane 8 na itachukua wanafunzi
wenye mahitaji maalumu ambapo tayari wameshapata waalimu 5 kwa ajili ya
kuanza kutoa elimu hiyo ambayo itakuwa shule ya mfano hapa Tanzania.
Amewataka
wazazi kutowaficha watoto wao wenye ulemavu bali watumie fursa
iliyojitokeza katika kuhakikisha wanawapatia elimu ambayo itawasaidia
katika kujenga msingi mzuri wa maisha
Kwa
upande wake mbunge wa Arumereru Mashariki John, Danielson Palanjo
amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha elimu inapewa kipaombele
hasa kwa watu wenye mahitaji maalumu kwa kuwa nao wana uwezo wa
kulitumikia taifa
Amesema
huduma ya elimu katika ambayo imeletwa wilayani hapo, italeta manuafaa
kwa jamii na kuwa mfano kwa huiduma ambazo kila mtu atazifaidi kwa kuwa
itakuwa tegemezi kwa kila mwananchi
Nae
mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru Bw. Emanuel Mkongo amesema
wao kama halmashauri bwanasubiri kukabidhiwa madarasa na pia
watahakikisha kila kitu kimekamilika ili kuweza kuruhusu wanafunzi
kuingia madarasani ambapo nao wana mchango mkun=bwa katika kuhakikisha
wanaungana na serikali kuendeleza watu wenye mahitaji maalumu
Hata
hivyo shule hiyo itakuwa na uwezo wa kuwa na wanafunzi 120 wenye
mahitaji maalumu bila ubaguzi na watapata huduma mabalimbali kulingana
na uwezo wao
Muonekano
wa Bwalo la Wanafunzi wenye mahitaji maalumu linalojengwa katika Shule
ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Chuo cha Ualimu Patandi,
Arumeru mkoani Arusha
Muonekano wa Jengo la Utawala la Shule ya Wanafunzi wenye mahitaji maalumu inayojengwa katika Chuo cha Ualimu Patandi.
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
No comments:
Post a Comment