Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa
Kijiji cha Mwiseni, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda
Mkoa wa Mara, katika Mkutano wa hadhara, uliofanyika Kijijini hapo, leo.
Lugola ameyataka Makanisa na Misikiti pamoja na Taasisi nyingine za
kiroho nchini zifanye uhakiki na endapo zitashindwa kufanya hivyo,
zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara,
Kangi Lugola, (kushoto), akimsalimia Mkazi wa Kijiji cha Mwiseni, Kata
ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, baada ya
kumaliza ya kuzungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara,
uliofanyika Kijijini hapo, leo. Lugola ameyataka Makanisa na Misikiti
nchini ifanye uhakiki na endapo yatashindwa kufanya hivyo, yatachukuliwa
hatua kwa mujibu wa sheria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
………………………………………..
Na Felix Mwagara, Mwibara (MOHA)
WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema Makanisa na Misikiti
nchini ambayo itashindwa kwenda kufanyiwa uhakiki itachukuliwa hatua kwa
mujibu wa sheria.
Waziri
Lugola ameyazungumza hayo katika Mkutano wa hadhara wa Wananchi wa
Kijiji cha Mwiseni, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda,
Mkoani Mara, leo, ambapo alifafanua kuwa; uhakiki huo ni lazima na
unalenga kuzifuatilia taasisi hizo za dini kujua utendaji wake wa kazi
kama unaendana na sheria za usajili.
Lugola
amesema Serikali haikuweza kuendelea na usajili wa Makanisa na Misikiti
pamoja na Taasisi za kiroho nchini, wakati kwa hivyo ikaona ifanye
uhakiki kwanza kwa lengo la kujua taasisi hizo zinaweza sawa na sheria
za usajili.
“Tuhakikishe
tunaendesha Makanisa na Misikiti na hizi taasisi za kiroho na kijamii
kwa mujibu wa masharti ambayo mmesajiliwa kufanya, na pale ambapo
utakuta, Kanisa lolote, Msikiti wowote, taasisi ya kiroho yoyote
inafanya shughuli zake kinyume ne kusajiliwa kwake, kujihusisha na mambo
ambayo hawaruhusiwi, sisi kama Wizara tumeapa kumsaidia Mhe. Rais
tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria na utaratibu,” alisema Lugola.
Aidha,
Waziri Lugola aliwatoa hofu wananchi kutokana na kuwepo kero ya
upatikanai wa vitambulisho vya taifa, alisema hakuna mwananchi
atakayekosa kitambulisho hicho na mwanzoni mwa wiki hii amewaelekeza
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kutoa namba kwa wakati ili
waweze kufanyiwa na usajili wa simu zao za mkononi.
“Narudia
tena, kitambulisho ni haki ya kila mwananchi na hakuna atakayekosa
kitambulisho cha taifa, pia nimewaelekeza NIDA waniletee takwimu za
Wilaya zote ili kujua ukubwa wa tatizo la usajili wa vitambulisho hivyo
unavyoendelea,” alisema Lugola.
Pia,
Waziri Lugola alisema Tanzania ina amani kwasababu inautamaduni wa kuwa
na amani, hivyo asitokee mtu akaharibu utamaduni huo ambao nchi
inaendelea kuhudumisha.
“Ndugu
zangu wana Mwiseni, Wana Mwibara, amani tulionayo ndiyo inatuwezesha
leo tunalima vizuri, tunavua samaki, leo tunakula vizuri, leo tunafanya
shughuli mbalimbali za maendeleo, hivyo tuendelee kuitunza amani hii,”
alisema Lugola.
Aliongeza
kuwa, Wizara yake kupitia Jeshi la Polisi ipo imara, Serikali ya Rais
Dkt. John Magufuli ipo imara na inaendelea kuwalinda Watanzania mahali
popote walipo nchini, na hakuna mtu atakaye ivunja amani hiyo.
Aidha,
Lugola aliwataka wananchi hao kuhifadhi vyakula vizuri ili kuepusha
janga la njaa kwa hapo baadaye na kusababisha wananchi kuja kuteseka kwa
ukosefu wa vyakula na kusababisha mateso katika familia.
“Tutunzeni
vyakula vyetu, msitumie hovyo, kuweni makini na matumizi ya vyakula,
sitaki nije kuona mnateseka na njaa, hakikisheni mnatunza vyakula kwa
ajili ya matumizi ya baadaye, ogopeni njaa kama ukoma,” alisema Lugola.
Lugola
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, ameanza ziara jimboni kwake ya
kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi
kupitia kufanya mikutano ya hadhara.
No comments:
Post a Comment