Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi
Kapulya Musomba akizungumza na wanahabari katika maonyesho ya Kimataifa
ya Biashara Sabasaba 2019 kuelezea mikakati mbali mbali ambayo shirika
limejipanga kuongeza mikakati ya upatikanaji wa gesi nchini Tanzania.
Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Muonekano wa Banda hilo.
Wananchi wakipata maelezo juu ya mfumo wa usambazaji gesi wakati
walipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC)
lililopo viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Saalaam.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa akipata
maelezo juu ya gari lililofungwa mfumo wa kutumia gesi asilia wakati
alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC)
lililopo katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wananchi
waliotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC)
wakiangalia gari lililofungwa mfumo wa kutumia gesi asilia.
Wafanyakazi wa TPDC wakiwa katika picha ya pamoja Kaimu Mkurugenzi Mhandisi Msomba.
Na Zainab Nyamka, Michuzi TV.
SHIRIKA
la maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) wamesema mpaka kufikia mwezi
Septemba mwaka huu watakuwa wameshafungua vituo vingi vya huduma ya gesi
kwa magari. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya
Petroli nchini (TPDC) Mhandisi Kapulya Musomba wakati wa maonesho ya 43
ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere
barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Musomba
amesema, mpaka sasa kuna kituo kimoja cha kuuzia gesi ambacho kipo
Ubungo ila mkakati wao ni kuwa na vituo vingi sana vitakavyotoa huduma
kwa wananchi. "Kuna kituo kimoja cha gesi ambacho kipo Ubungo ila
mikakati tuliyokuwa nayo kufikia Septemba mwaka huu tutakuwa na vituo
vingi vya kuuzia gesi, " amesema Musomba.
Ameeleza
kuwa, TPDC wapo kwenye mkakati wa kuongea na wamiliki wa Mwendokasi na
kuwashauri kuleta magari yatakayokuwa yanatumia gesi ili kupunguza
gharama za uendeshaji ikiwemo na kushusha bei kwa abiria. Akielezea
faida za Gesi, Masumbo amesema mpaka sasa uzalishaji wa umeme unategemea
asilimia 50 ya gesi na kupelekea kupungua kwa changamoto ya kukatika
kwa umeme.
Musumbo
amesema, wameshaanza kusambaza gesi katika maeneo ga Mlalakuma,
Mikocheni, Mbezi, Mwenge na wapo kwenye njiani kusambaza Mkoa wa Mtwara
na Lindi na hiyo ni kwa matumizi ya kawaida majumbani. Ameshauri, watu
kuagiza magari yanayotumia gesi, au yanayotumia vyote ili kupunguza
gharama za uendeshaji.
No comments:
Post a Comment