Na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Watumishi
wa Wizara ya Fedha ya Mipango wametakiwa kuzingatia Sheria na Kanuni za
Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao. Wito huo umetolewa na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James wakati wa kikao cha watumishi
wa Wizara hiyo.
Bw.
James alisema kuwa watumishi wote wanawajibu wa kufanya kazi kwa
ufanisi na weledi na kwa kuzingatia nidhamu, maadili, sheria, kanuni na
taratibu za utumishi wa Umma.
“Ni
wajibu wa kila mtumishi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wote
wanaohitaji huduma katika Wizara yetu” Alisema Bw. James.
Aidha
Bw. James aliwapongeza Watumishi wa Wizara hiyo kwa kazi wanazozifanya
hususan kazi ya uandaaji wa Bajeti Kuu ya Serikali iliyopishwa na Bunge
hivi karibuni na kuwataka waendelee kutoa ushirikiano katika utekelezaji
wa Bajeti hiyo.
Kwa
upande wa Watumishi wa Wizara hiyo waliupongeza uongozi wa Wizara hiyo
kwa kutenga muda wa kuzungumza nao na kusikiliza changamoto mbalimbali
zinazo wakabili pamoja na kuzitolea ufafanuzi.
Waliahidi kutatekeleza maelekezo yote aliyotolewa kwa uadilifu ili kuongeza ufanisi wa kazi kwa maendeleo ya nchi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, akifungua kikao
cha Watumishi wa Wizara hiyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la
maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma, Jijini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu
akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James (hayupo
pichani), wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika
Jijini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Adolf Ndunguru akifafanua
jambo wakati wa kikao Kati ya Viongozi na Watumishi wa Wizara hiyo
kilichofanyika Jijini Dodoma, ambapo Watumishi waliaswa kufanya kazi
kwa bidii na weledi.
Mhasibu
Mkuu wa Serikali, Bw. Francis Mwakapalila akijibu hoja katika kikao
kati ya viongozi na Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango
kilichofanyika Jijini Dodoma.
Kamisha
wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Mgonya Benedicto akichangia
hoja wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika Jijini
Dodoma.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha na Mipango,
Bw. Alfred Dede akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoibuliwa wakati
wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo ambacho kiliongozwa na Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Bw. Doto James (hayupo pichani), Jijini Dodoma.
Katibu
wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Umma (TUGHE) wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bi. Jenjel James akichangia mada katika kikao cha viongozi na
Watumishi wa Wizara hiyo ambapo Watumishi walitakiwa kuzingatia Sheria
na Kanuni za Utumishi wa Umma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, akisisitiza jambo
wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo, Jijini Dodoma.
Baadhi
ya Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara ya Fedha na Mipango
wakifuatilia kwa karibu kikao cha viongozi na Watumishi wa Wizara hiyo,
kiliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James (hayupo
pichani), Jijini Dodoma.
Baadhi
ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza hoja mbalimbali
zilizokuwa zikitolewa katika kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo Jijini
Dodoma.
Mtumishi
wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Hilder Rugemalira akitoa hoja wakati
wa kikao kati ya viongozi na Watumishi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment