Dar
es Salaam, 30/08/2019.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MOI Profesa Charles Mkony leo ameongoza kikao cha kwanza cha bodi mpya ya MOI ambapo wajumbe wamepata fursa ya kukutana na menejimenti pamoja na kukagua maeneo ya kutolea huduma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MOI Profesa Charles Mkony leo ameongoza kikao cha kwanza cha bodi mpya ya MOI ambapo wajumbe wamepata fursa ya kukutana na menejimenti pamoja na kukagua maeneo ya kutolea huduma.
Prof.
Mkony ameongoza wajumbe hao kujadili mipango, mikakati pamoja na kupitia
taarifa mbalimbali za Taasisi ambazo zimewasilishwa zinazolenga kuendelea
kuboresha utoaji wa huduma bora kwa watanzania.
Pamoja
na Mwenyekiti wa bodi hiyo mpya Prof. Charles Mkony na Katibu Dkt Respicious
Boniface wajumbe wengine ni Bi Deodatha Makani, Dkt Amani Malima, Bw. Charles
Beida, Dkt Pilly Chillo, Dkt Tuhuma Tuli, Dkt Petronila Ngiloi, Dkt Pern Tellya
na Dkt Lusisyo Mwakaluka.
Aidha,
Prof.Mkony amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kuongoza bodi ya wadhamini ya
Taasisi kubwa ya MOI.
“Ikiwa
ni kikao cha kwanza nimshukuru sana Mh Rais kwa nafasi hii, ameonyesha imani
kwangu na kwa wenzangu hivyo ni jukumu letu kufanya kazi kwa bidii na kwa
weledi ili Taasisi hii tegemeo iendelee kutoa huduma bora” Alisema Prof. Mkony
Kwa
upande wake ,Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema ujio wa
bodi mpya wa wadhamini MOI utaleta mageuzi makubwa katika utoaji wa huduma
pamoja na kuendelea kuboresha na kuanzisha huduma mpya sawa na zile za mataifa
ya Ulaya na India.
Baada
ya kukamilisha ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma MOI wajumbe wa bodi
mpya ya wadhamini MOI wameipongeza Serikali kwa ukwekezaji mkubwa iliyoufanya
kwenye miundombinu, vifaa, majengo na wataalamu na kuahidi kuifanya MOI
kuendelea kuwa Taasisi bora zaidi barani Afrika.
No comments:
Post a Comment