Wadau wa mazao ya nafaka, wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe. Japhate Hasunga wakati akihutubia mkutano wa siku mbili wa Wafanyabiashara wa Nafaka Ndani na Nje ya Nchi kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam
Mkutano
wa siku mbili wa Wafanyabiashara wa Nafaka Ndani na Nje ya Nchi umefunguliwa na
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Agosti 29, 2019.
Mkutano
huo ambao umewajumuisha wasindikaji, wasafirishaji na wamiliki wa maghala ya
nafaka Lengo lake ni kuangalia fursa zilizopo kwenye tasnia ya nafaka na jinsi
ya kuzifikia ikiwa ni pamoja na masoko.
Mhe. Waziri Hasunga.
Akizungumza
na washiriki wa mkutano huo uliowakutanisha
wadau kutoka mikoa mbalimbali nchini,
Mhe. Hasunga ambaye alifuatana na Manaibu wake, Mhe. Husein Bashe, na Mhe.
Omary Mgumba alisema mkutano huo utatoa fursa kwa wajumbe kuelimishwa kuhusu
fursa ya biashara ya mazao ya nafaka katika soko la Afrika, uwezo wa Tanzania
kuzalisha na nafasi ya wafanyabiashara kushiriki kikamilifu lakini pia
washiriki watapata fursa ya kujifunza athari za upotevu wa mazao ya nafaka
baada yamavuno na mkakati wa serikali kudhibidi hali hiyo.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akihutubia mkutano huo.
“Kitaalamu
wanasema utafiti uliofanyika Tanzania na
nchi nyingi za Kusini asilimia 40 ya mazao yote yakiwemo ya nafaka
yanapotea baada ya mavuno kwa kuharibika na matatizo mengine, hii haikubaliki
mkulima amewekeza, amevuna halavu mazao yake yanaharibika, lazima tuwe na
mkakati wa kuzuia hali hii.” Alitoa hakikisho Mhe. Waziri Hasunga na kuongeza.
Kulingana
na uzalishaji uliopo, nafaka nyingi kama mahindi mtama na nafaka nyingine
huhifadhiwa katika kiwango kisichoridhisha hali hii huchangia kupoteza ubora wa
nafaka na hatimaye huchangia kuzorota kwa ustawi wa afya zetu, alifafanua zaidi
Mheshimiwa Waziri.
Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
Dkt.Hoseana Lunogelo, akiwasilisha mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage
facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).
Alisema
Agosti 1, mwaka huu kwenye sherehe za Nanenane kwenye viwanja vya Nyakabindi
Mkoani Simiyu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganow a Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan alizindua mkakati wa namna ya kupambana na kudhibiti upotevu wa
mazao baada ya mavuno.
Katika
utafiti wake ilioufanya hivi karibuni Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii
(ESRF) chini ya Mradi wa Rapid Response
Implementation Support to the Ministry of Agriculture and Agriculture Sector
Lead Ministry (RARIS) unaofadhiliwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation umebaini kuwa hali ya maghala
mengi ya watu binafsi hayatoi taarifa serikalini na hii ni kutokana na mfumo wa
sasa wa maghala.
Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
Dkt.Hoseana Lunogelo, akiwasilisha mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage
facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).
Akitoa
mada kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage
facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses),
Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
Dkt.Hoseana Lunogelo alisema ESRF ilifanya utafiti wa hali (status) ya maghala
nchini na kubaini kuwa maghala ya watu binafsi hayalazimiki kisheria kutoa
taarifa serikalini kuhusu nini kimehifadhiwa na kiasi gani cha nafaka
kilichohifadhiwa ndani ya maghala hayo na hali hii serikali inategemea tu
maghala ya Serikali yaani (Public Storage
Facilities ) kupitia Werehouse Reseat
Regulatory Board ili kujua takwimu za hali ya chakula nchini.
Bi.
Margareth Nzuki (katikati), akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF
akifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inawasilishwa na Dkt. Bunogelo
kuhusu utafiti ambao ulifanywa na Taasisi hiyo kuhusu mahusiano kati ya maghala (Storage
facilities na upotevu wa mazao baada ya mavuno, post harvest losses).
Alisema
hii ni changamoto kubwa, kama serikali inapata taarifa kutoka kwenye maghala
machache sana nchini na yale mengi haipati taarifa zake, maana yake Serikali
haiwezi kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na upatikanaji wa chakula nchini na
hiyo ina athari mbaya kwenye usalama wa chakula na pia ina athari mbaya pia
kwenye biashara.” Alsiema Dkt. Lunogelo.NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Mkuurgenzi Mtednaji wa Benki ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw.Japhet Justine akipiga makofi wakati mkutano huo ukiendelea
“Kwa
sasa kuna maghala 3,430 yaliyopo kati ya hayo ni 185 tu ndiyo kuna uhakika wa
kupata tawimu endapo zitahitajika lakini yaliyosalia huwezi kupata takwimu hizo
kwa sababu hakuna sheria inayowalazimisha kufanya hivyo.” Alifafanua Dkt.
Lunogelo.
Mjumbe akifuatilia kwa makini mkutano huo.
Mjumbe akifuatilia kwa makini mkutano huo.
Bi.Margareth
Nzuki (kushoto), kutoka ESRF akibadilishana mawazo na Bi. Vumilia L.
Zikankuba kutoka Wizara ya Kilimo wakati wa mkutano huo.
Mshiriki akitoa maoni yake.
Oswald
Mashindani (kushoto), kutoka ESRF akizunhumza jambo mbele ya Katibu
Mkuu (mstaafu) Wizxara ya Fedha, Bw. Paniel Lyimo (katikati) wakati wa
mkutano huo.
Mhe. Hadsunga (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na manaibu waziri makatibu wakuu na Mwenyekiti wa TPSF.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo unaofikia kilele leo Agosti 30, 2019. |
No comments:
Post a Comment