Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimkabidhi Funguo ya Pikipiki Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith S.
Mahenge Baada ya kuzindua rasmi Mradi wa kutokomeza vitendo vya
Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo
ya Masoko kwa ajili ya kuongeza Chachu ya kurahisisha Usafiri katika
kufanikisha zoezi hilo, Jumla ya Pikipiki 14 zilitolewa kwa Mkoa wa
Dodoma . Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya
Nyerere Square Jijini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiangalia Bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Wajasiriamali Wanawake
katika Mkoa wa Dodoma alipotembelea Mabanda ya Maonesho kwenye Uzinduzi
wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya
Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo
Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akionesha Bango Juu kama ishara ya Uzindua rasmi Mradi wa kutokomeza
vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto
katika maeneo ya Masoko pamoja na ugawaji wa Pikipiki 14 kwa Maafisa wa
Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino Dodoma kwa ajili
ya kuongeza kurahisisha Usafiri katika kufanikisha kutokomeza Ukatili
na Unyanyasaji kwa Wanawake na watoto . Hafla hiyo imefanyika leo Julai
30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Katikati
Mwenyekiti wa ALAT Taifa na Meya wa Manispa ya Shinyanga Mhe.
Gulamhafeez Z. Mukadam na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Baadhi
ya Wafanyabiashara wa Masokoni Wanawake na Wanancho wa Dodoma,
wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akihutubia kwenye Hafla ya Uzinduzi wa
Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya
Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo
Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Mratibu wa Umoja wa Mataifa Tanzania Alvaro Rodriquez
walipokutana kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya
Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo
ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya
Nyerere Square Jijini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshuhulikia Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake (UN WOMEN)
Bibi. Hadon Addou walipokutana kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa
kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na
Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019
katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa ALAT Mhe Gulamhafeez Mukadam,akizungumza na Wafanyabishara Wanawake
wa Masokoni na Wananchi wa Dodoma kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa
kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na
Watoto katika maeneo ya Masoko. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019
katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akihutubia Wafanyabishara Wanawake wa Masokoni na Wananchi wa Dodoma
kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji
na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko.
Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere
Square Jijini Dodoma.
Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
akizungumza na Wafanyabishara Wanawake wa Masokoni na Wananchi wa Dodoma
kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji
na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko.
Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika Viwanja vya Nyerere
Square Jijini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akikata Utepe kuzindua rasmi Mradi wa kutokomeza vitendo vya Unyanyasaji
na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake na Watoto katika maeneo ya Masoko
pamoja na ugawaji wa Pikipiki 14 kwa Maafisa wa Maendeleo ya Jamii wa
Halmashauri ya wilaya ya Chamwino Dodoma kwa ajili ya kuongeza
kurahisisha Usafiri katika kufanikisha kutokomeza Ukatili na Unyanyasaji
kwa Wanawake na watoto .
Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30,2019 katika
Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Makamu
wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema watu wanatumia
matusi ni watu waliokosa malezi kwa namna tofauti tangu wakiwa wadogo
hivyo kuitaka Jamii ya Watanzania kutumia nguvu nyingi katika malezi ya
watoto ili kuepukana na athari za ukosefu wa malezi ukubwani.
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo jijini Dodoma katika
hotuba yake ya uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza vitendo vya unyanyasaji
na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo ya masoko na
zoezi la ugawaji wa pikipiki kwa waataalam wa maendeleo ya Jamii leo
Jijini Dodoma.
Aidha
Makamu wa Rais amekemea wanaume wanaotumia lugha ya matumisi katika
maeneo ya masoko kuwa yanasabababisha wakina mama wafanya biashara
Sokoni kukosa uhuru na hata kushindwa kuleta watoto wao sokoni kwa ajili
ya kuwasaidia kwa kutopenda vijana wao kusikia lugha isiyokuwa na
maadili.
“Mnawazalilisha
wanawake kwa kuwatukana matusi kwa kutumia viungo vyao, kuwashika au
kuwapapasa bila idhini yao kwanini nyie wanaume msishikane wenyewe
vitendo vya kuwazalilisha wanawake havikubaliki kabisa’’. Alisisitiza
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika
hotuba yake hiyo Makamu wa Rais wa Tanzania amesema vitendo hivyo vya
ukatili havikubaliki na ndio maana ya ilani ya Uchaguzi ya Chama cha
Mapinduzi ibala ya 168 c inasema wanawake wanayo haki ya kulindwa dhidi
ya unyanyasaji wa aina yoyote ile hivyo hatua za kukomesha vitendo vya
ukatili dhidi yao ni utekelezaji wa ilani hiyo.
Pamoja
na kukemea vitendo hivyo Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan amewataka wanaume wanaonyanyaswa Kijinsia wasione aibu bali watoe
taarifa kwenye dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi ili Serikali iweze
kupata takwimu sahihi ili iweze kufanyia kazi chanagamoto hiyo.
Aidha
Makamu wa Rais amehoji wanawake walio katika Kamati ya Soko kwanini
wanafumbia macho vitendo vya ukatili ili hali wao ni viongozi watoa
maamuzi sokoni hapo na kuonya kuwa uenda na wao wanachangia kuendelea
kuwepo kwa ukatili katika maeneo ya sokoni.
Makamu
wa Rais amewataka viongozi wa masoko nchini kuhakikisha wanafanyia kazi
tabia ya watoto wadogo kufanya biashara sokoni kwa lengo la kusaidia
familia na kuutaka uongozi wa soko kuwahoji na kuwarudisha shuleni ili
kusaidia kukata mnyororo wa umasikini wa familia kwani mtoto akipata
elimu inamsaidia kutumia elimu yake kupambana na umasikini.
Kwa
upande wake Waziri wa Afya, MAendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu amemwomba Makamu wa Rais kuagiza Halmashauri zote
nchini kuacha kutoa kiwango kidogo cha mikopo kwa akina na mama na
waongeze kiwango cha fedha ili wakinamama wapate miradi ya maana ya
biashara kupitia makato ya 4% ya mapato ya kwa Halmashauri.
“Unakuta
kikundi cha akina mama watano wapewa mkopo wa laki tano nakugawana
fedha kidogo hii ni pesa gani ndio maana wakina mama wanaishia kuila na
kushindwa kufanya marejesho kwa kuwa fedha hii inakuwa haitoshi kufanya
chochote’’ Aliongeza Waziri Mwalimu.
Naye
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu
amesema Wizara kwa kushirikiana na wadau wataendelea kutafuta na kugawa
Pikipiki kwa Mikoa mingine baada ya Mkoa wa Dodoma ili kuwawezesha
Maafisa Maendeleo nchini kutoa elimu kwa jamii kuhusu vitendo vya
ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Dkt.
Jingu amesema kuwa Wizara imetoa pikipiki 25 kwa mkoa wa Dodoma na
mapema mwezi ujao itatoa pikipiki kumi na tano kama hizo kwa Mkoa wa
Rukwa ili kuwawezesha Maafisa Maendeleo Mkoani humo kutumia usafiri huo
kuelimisha wananchi kuhusu ukatili na unyanyasaji dhidi ya Wanawake na
Watoto.
Naye
Beatrice Siame ambaye ni Mwakilishi wanawake Soko la Majengo ameiomba
Serikali kusimamia usawa wa kijinsia katika maeneo ya kazi ili wanawake
waweze kunufaika na kuwezeshwa kiuchumi lakini pia akibainisha kuwa
changamoto ya soko ya bidhaa zao ni kikwazo katika kumwendeleza mwanamke
kiuchumi.
Uzinduzi
wa Mradi wa kupinga unyanyasaji na udhalilishaji wanawake kijinsia
katika Masoko ni hatua muhimu ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa
Kutomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto unaolenga
kutokomeza vitendo vya ukatili Nchini kwa 50% ifikapo 2022.
No comments:
Post a Comment