Hospitali
ya Rufaa ya Kanda ya Bugando (BMC) imefanikiwa kuokoa zaidi ya Shilingi
bilioni mbili kwa wananchi wa kanda ya ziwa kusafiri kwenda jijini Dar
es Salaam kupata matibabu ya saratani kila mwaka.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo Prof. Abel Makubi
wakati akiongea na Maofisa habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake
waliokuwepo jijini Mwanza kwa ajili ya kujionea mafanikio ya utoaji
huduma za afya kwa wananchi.
Prof.
Makubi alisema kuwa kuanza kwa tiba ya saratani katika Hospitali ya
Kanda Bugando imesaidia kuokoa kiwango cha fedha hizo kutoka kwa
wananchi wa kanda ya ziwa ambapo awali iliwalazimu kusafiri hadi Jijini
Dar es Salaam kupata huduma hizo kwenye Hospitali ya Saratani ya Ocean
Road.
“Tunaishukuru
Wizara ya Afya ambayo ilitupatia kiasi cha Shilingi bilioni 5.5 kwa
ajili ya kujenga jengo la saratani. Kama hospitali tumeweza kununua
mashine nne za mionzi na dawa kwa kushirikiana na wafadhili wengine".
Aidha,
alisema, hivi sasa asilimia 90 ya wagonjwa hawapelekwi wanapata huduma
hapa hivyo kuwaondolea adha ya kusafiri na kupata huduma mbali wananchi
wa kanda ya ziwa ambapo awali zaidi ya asilimia 50 ya wagonjwa wa
saratani wa Ocean Road walikuwa wakitoka kanda hiyo.
Naye
Mtaalam wa Tiba Mionzi wa Idara ya Saratani wa BMC, Alex Mpugi alisema
kabla ya mashine hizo walikua wakitoa huduma za saratani kwa kutumia
kemikali.
"Naomba
nitoe wito kwa wananchi hususan wanawake kujitokeza kufanya uchunguzi
wa saratani ya shingo ya uzazi na matiti kila siku ya Jumanne na
Alhamis".Alisisitiza Mpungi.
Kwa
upande wa Upasuaji Mkurugenzi wa Upasuaji Dkt.Fabian Massaga alisema
kuwa,Hospitali imefanikiwa kufanya ukarabati na upanuzi wa vyumba vya
upasuaji kutoka vyumba sita hadi kumi na tatu ambapo vyumba viwili
hutumika kwa upasuaji wa dharura na kimoja kwa ajili ya upasuaji kwa
akina mama wajawazito.
Aliongeza
kuwa kwa upande wa upasuaji wameweza kuongeza idadi ya wagonjwa kutoka
ishirini na tano hadi hamsini na hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa
wengi waliokuwa wanasubiri upasuaji kwa miezi mitatu lakini hivi sasa
wanafanyiwa upasuaji ndani ya wiki moja.
Hata
hivyo Dkt. Massaga alisema upanuzi huo umeendana na ununuzi wa vifaa
vipya na vya kisasa ikiwemo vitanda vya kufanyia upasuaji, taa maalumu
za vyumba vya upasuaji na mashine za kisasa kabisa za kutolea dawa ya
usingizi. Vifaa hivi vimeagizwa moja kwa moja viwandani kwa takribani
Shilingi bilioni 1.4 badala ya Shilingi bilioni 3 kama wangenunua kwa
wauzaji hapa nchini.
Mtaalam wa mionzi Alex Mpugi akitoa maelezo jinsi mashine ya mionzi inavyofanya kazi
Mashine ya kisasa ya kutambua(kupanga) sehemu inayotakiwa kupatiwa mionzi iliyoko kwenye hospitali ya kanda ya rufaa Bugando
Mfizikia
Tiba wa Idara ya Saratani katika hospitali ya Bugando Prof. Pradumna
Chaurassia akiwaelekeza maofisa habari jinsi wanavyozuia eneo jingine
ambalo halijaathirika na saratani isipate mionzi pia saratani isienee
mahali pengine
Mfizikia
Tiba wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Bugando Prof. Pradumna
Chaurassia akiwaelekeza maofisa habari jinsi wanavyozuia eneo jingine
ambalo halijaathirika na saratani isipate mioni piasaratani isienee
mahali pengine
Mkurugenzi
wa upasuaji wa BMC Dkt. Fabiani Massaga akifafanua jambo wakati
maofisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake walivyotembelea idara
hiyo ambapo hivi sasa wamepunguza idadi ya wagonjwa kusubiri upasuaji
kutoka miezi mitatu hadi ndani ya wiki moja
Picha
ya pamoja ya maofisa habari kutoka wizara ya afya na taasisi zake mara
baada ya kutembelea idara ya upasuaji na kujionea maboresho makubwa
ikiwemo upanuzi wa vyumba vya upasuaji kutoka sita hadi kumi na tatu
pamoja na vifaa na vifaa tiba vya kisasa.
No comments:
Post a Comment