Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akisoma hotuba ya
ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi
lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere wa Chuo cha Mipango
jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Maliasili
katika Umoja wa Ulaya (EU) ambao ni wafadhili wa miradi ya Eco
villages, Jenny Correia Nunes akizungumza wakati wa Kongamano la wadau
wa mabadiliko ya tabianchi.
Mkuu wa Chuo cha Mipango, Profesa
Hozen Mayaya akitoa neno la kumkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene
kufungua Kongamano la wadau wa mabadiliko ya tabianchi.
Sehemu ya washiriki wa Kongamano
la wadau wa mabadiliko ya tabia nchi lililofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Mwalimu Nyerere wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene alkiangalia bidhaa
mbalimbali zilizozalishwa na wanufaika wa Miradi ya Eco villages
yaaliyokuwa yakioneshwa wakati wa Kongamano
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa
na Mkuu wa Kitengo cha Maliasili katika Umoja wa Ulaya (EU), Jenny
Correia Nunes na Mkuu wa Chuo cha Mipango, Profesa Hozen Mayaya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akifungua
Kongamano la wadau wa mazingira katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu
Nyerere Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (waliokaa
katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na
washiriki wa Kongamano la wadau wa mabadiliko ya tabianchi jijini
Dodoma.
………………..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene amesema mabadiliko
ya tabianchi ni janga la kitaifa na dunia kwa ujumla hivyo kila mtu
anao wajibu wa kutunza mazingira kwa kupanda miti.
Mhe. Simbachawene amesema hayo leo
Septemba 6, 2019 wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Kupambana na
Mabadiliko ya Tabianchi lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu
Nyerere wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Alisema kuwa changamoto ya
mabadiliko ya tabianchi imesababisha mabadiliko ya misimu na hivyo
kuleta athari kwa wanadamu kushindwa kuendesha shughuli za kilimo.
“Hali hii imechangia sana
kubadilisha misimu mbalimbali kwani baadhi ya mazao tuliyozoea
hatuyapati tena kutokana na kukosekana kwa mvua na pia mifugo yetu
inakosa malisho yote haya yanasababisha kwa mabadiliko ya tabianchi,”
alitahadharisha.
Waziri Simbachawene alibainisha
kuwa takwimu zinaonesha zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wanategemea
mvua kufanya shughuli za kilimo lakini Tanzania inakabiliwa na
mabadiliko ya tabianchi.
Aliongeza kuwa sehemu kubwa ya
nchi ilikuwa na ukame ambao ulichangia uzalishaji mdogo wa mazao na
Serikali lichukua hatua madhubuti za kukabiliana na changamoto hiyo kwa
kuwataka wananchi kutumia chakula kwa uangalifu, kupanda mazao
yanayohimili ukame, kuuza mifugo ili kununua chakula na kuhifadhi
Waziri Simbachawene alibainisha
kuwa kwa mujibu wa sheria suala la utunzaji wa mazingira si tu la Ofisi
ya Makamu wa Rais bali ni la kila mmoja ambapo taasisi zingine za
Serikali na zisizo za Serikali zinapaswa kushiriki ili kuhakikisha
tunaondokana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.
Aidha Waziri Simbachawene
alipongeza miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) ya kukabiliana
na mabadiliko ya tabianchi ya Eco villages ambayo imetekelezwa katika
maeneo kadhaa nchini na kusema itapunguza makali ya mabadiliko ya
tabianchi.
Alisema kuwa miradi hiyo
iliyotekelezwa imeweza kuwajengea uwezo wananchi kuhusu namna ya kufanya
shughuli mbadala pale panapokuwa na changamoto za kimazingira kama hizo
na hivyo kujikimu kimaisha.
Kongamano hilo limeandaliwa kwa
ushirikiano wa Chuo cha Mipango Dodoma kwa kushirikiana na taasisi
mbalimbali likil;enga kujadili taarifa za miradi mbalimbali ya
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
No comments:
Post a Comment